Rais
Jakaya Kikwete kulia akimpokea Balozi wa Japan nchini Masaki Okada
(kushoto). Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi(WAMA –
Nakayama) wakati walitembelea shule hiyo leo iliyopo wilayani
Rufiji mkoa wa Pwani.
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwalimu wa masomo ya Kiingereza na
Uraia wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya watoto yatima na wanaoishi
katika mazingira hatarishi(WAMA –
Nakayama) Sophia Shafii wakati alipotembelea shule hiyo leo
iliyopo wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete( wa tatu kushoto) na Balozi wa Japan nchini
Masaki Okada( wa pili kulia) wakitia saini mkataba wa msaada wa
kutayarisha vifaa vya maabara, ujenzi wa zahanati na kutoa mtambo wa
maji wa kutumia jenereta wenye thamani milioni 170 kwenye Shule ya
Sekondari ya Wasichana ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira
hatarishi(WAMA – Nakayama) . Kulia wa kwanza ni Rais Jakaya Kikwete na
kushoto wa pili ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo ,Ramadhani Dau .
Kushoto wa kwanza ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Suma Mensah. Hafla
fupi hiyo iliyafanyika leo katika shule hiyo iliyopo wilayani
Rufiji mkoa wa Pwani.
Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)