Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa majadiliano ya Jumuiya ya Madola.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia majadiliano; mwenye tai nyekundu ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile.
Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dkt. Philip Mpango, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile, Kamishna wa Sera Bw. Beda Shallanda na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa majadiliano ya mkutano wa madola.
Mwenyekiti wa majadiliano ya mkutano wa Madola Bw. Sheku Sesay akifafanua jambo.
Wakati mikutano
mingine ikiendelea hapa mjini Washington DC, Tanzania pia inashiriki katika mkutano
wa Jumuiya ya Madola ambao utafanyika kwa siku mbili mfululizo. Mkutano huu
unahudhuriwa na wajumbe wote ambao ni nchi wanachama.
Katika mkutano huo
kikubwa kilichojadiliwa ni kuhusiana na suala zima la biashara, ni namna gani
biashara inaweza kufanyika na kwamba nchi zetu haziko vizuri sana katika uwanja
huu wa kimataifa. Katika mkutano huo walijadili ni jinsi gani wanaweza
kufanikisha lengo la kuanzisha mfuko ambao utatumika kusaidia biashara ‘trade
facilitation’.
Katika majadiliano
yaliyokuwa yakifanyika wajumbe wengi walipenda kujua kwamba ni tofauti
gani mfuko huo mpya utaleta ili nchi zetu ziweze
kunufaika. Hiki ni kitu kikubwa zaidi kilicho wagusa wajumbe wengi.
Akizungumza na
vyombo vya habari Dkt. Silvacius Likwelile ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
ambaye alisema kuwa”katika mkutano huu jambo ambalo limezungumziwa sana ni kuhusu kuondoa
vikwazo ambavyo mara nyingi tunawekewa ili kufikia masoko katika ulimwengu”.
Aliendelea kusema
kuwa, ni imani yetu kwamba tume ya madola itafanyia kazi masuala hayo ili
hatimaye tuwe na msimamo mmoja wa kuweza kusaidia ukuaji wa biashara katika
nchi zetu.
Mkutano huu
utaendelea tena kesho na inategemewa utakuwa na mafanikio makubwa.
Imetolewa na:
Ingiahedi
Mduma
Msemaji
Mkuu
Wizara
ya Fedha
Washington
D.C
08/10/2013
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)