Baadhi ya vijana wakiwa wamebeba bango lililokuwa na ujumbe uliosema;
“Tutazika mpaka lini Kizuiani?”
“Tutazika mpaka lini Kizuiani?”
………………………………………………………………………..
NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM
Wakazi
wa Kizuiani Mbagala jijini Dar es Salaam, jana walizua vurugu na kuziba
kwa muda wa saa mbili barabara ya Kilwa na kusababisha magari mengi
kushindwa kuendelea na safari zao kisa kikiwa Mwanafunzi Adina Seleman
(11) wa darasa la 5 kugongwa na gari aina ya Scania na kufariki papo
hapo.
Tukio hilo lilitokea saa 5.45 asubuhi wakati mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Msingi Kibondemaji akivuka barabara katika eneo hilo. Wakazi hao walizusha vurugu hizo ikiwa ni njia ya kuishinikiza Wakala wa
Baraba nchini, Tanroad kuweka matuta ili kuzuia ajali zinazotokea mara
kwa mara katika eneo hilo.
Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa wa Kizuiani, Mashaka
Selemani, watu 30 wamepoteza maisha kwa ajali katika eneo hilo tangu
barabara hiyo ikamilike mwaka 2009.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo aliyekuwepo katika zoezi la kuwatawanya vijana walioziba barabara hiyo kwa magogo, kuchoma matairi moto na mawe akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio alisema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha uvunjifu wa sheria.
Kiondo alitoa rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kufikia muafaka wa
jambo lolote kwa kukaa mezani badala ya kuleta vurugu kama zilizotokea
Mbagala. Vijana wa Kizuiani wakichoma matairi moto katikati ya barabara kuzuia magari yasipite. Kijana huyu ambaye hakufahamika jina lake, akiwa ameinama na kunyosha mkono juu wakati askari polisi walipokuwa wakipiga mabomu ya machozi kuwatawanya vijana waliokuwa wakileta vurugu eneo la tukio.
Maaskari wakiwa katika eneo la tukio. Askari wa Ulinzi Shirikishi wa Mbagala wakimbeba msobemsobe ili kumuingiza ndani ya gari la polisi mmoja wa vijana aliyehisiwa alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakileta vurugu.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi Mbagala, Jonathan Shanna aliyesimama akiwapa maelekezo askari waliokuwa ndani ya gari wakati wa oparesheni ya kuwatawanya vijana waliokuwa wakifanya fujo.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)