Mhandisi Magessa akielezea mfumo huo wa jua
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi akifungua mafunzo mjini Bagamoyo.
………………………………………………………………………….
Na Andrew Chale, Bagamoyo
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo,
Ahmed Kipozi amewataka wananchi wa wilaya hiyo hasa vijijini
kuchangamkia fursa ya kuweka umeme nuru utokanao na jua maalufu kama
sola, ilikuboresha maisha yao na maendeleo kwa ujumla.
Kipozi alisema hayo mjini hapa
juzi wakati wa hafla ya kufungua mafunzo maalumu ya umeme huo kwa
mafundi umeme, wadau na wauzaji wa vifaa vya umeme na vijana mbalimbali
ndani ya wilaya hiyo ambapo mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA).
Akielezea kufarijika na mafunzo
hayo ndani ya Wilaya yake, Kipozi alisema “Ni fursa ya kipekee kwa
wanamafunzo kutumia ujuzi huu kwani utaboresha maisha yenu na pia kwa
vijiji vitanufaika na umeme huu wa nuru” alisema.
Na kuongeza kuwa, kwa fursa
hiyo, anaamini matumizi ya kukata miti hovyo itapungua na baadala yake
wananchi watanufaika na huduma hiyo endapo wataichangamkia.
“Nawaomba wananchi hasa mulio
vijijini kuchangamkia fursa hii ya umeme nuru, pia nawapongezeni
wakufunzi na wandaaji kwa kuja muda muafaka kwani mafunzo haya ni
mipango endelevu ambayo itasaidia kusambaza teknolojia ya nishati
mbadala vijijini sambamba na kuwahamasisha wananchi kutumia nishati
zitokanazo na teknolojia ya nishati jadilifu” alimalizia Kipozi.
Kwa upande wake, mkuu wa mafunzo
hayo ya umeme nuru, Mhandisi, Finiasi Magessa alisema mafunzo hayo
yatasaidia kuboresha maisha ya watanzania mbalimbali hasa wa vijijini
ilikufikia malengo ya MKUKUTA, ili kila Mwananchi apate umeme wa uhakika
na gharma nafuu ifikapo 2015.
Aidha, wanamafunzo wanatarajia
kufaanya kwa vitendo kwa kufunga umeme nuru katika shule na nyumba za
walimu za Sekondari Kiwangwa, Matipwili na Kibindu, huku mafunzo hayo
yakitaraajia kumalizika Novemba 7, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)