Viongozi wa Tanzania ukisikiliza kwa makini uongozi wa MCC hawapo pichani wakati wa majadiliano. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Jamhuri ya Muungano Dkt. Servacius Likwelile, Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula, Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa, Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Yusuph Mzee, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa.
Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano na MCC mjini Washington, kutoka kulia ni Kamishna wa Fedha za Nje Jamhuri ya Muungano Bw. Said Magonya, Kamishna wa Fedha za Nje Zanzibar, Bi. Bihindi Nassor, Naibu Ganana wa BOT Dkt. Natu Mwamba pamoja na Mkurugenzi wa Mipango Zanzibar.
Ujumbe wa Tanzania na Viongozi wa MCC katika majadiliano.Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi Eva Valerian – Washington DC
Wakati Mikutano ya
mwaka ya Shirika la fedha la kimataifa na makundi ya benki ya Dunia ikiendelea
hapa mjini Washington DC, Ujumbe kutoka Tanzania watumia nafasi hiyo kukutana
na Uongozi wa Millenium Challenge Corporation (MCC) kwa madhumuni ya kujadili mafanikio
yaliyopatikana kutokana na shirika hili
la Marekani. MCC awamu ya kwanza ilisaidia sana miradi mbalimabli Tanzania,
ambapo walitoa dola milioni 698 ambayo ilielekezwa katika miradi ya barabara,
umeme, maji pamoja na miradi ya barabara Zanzibar pamoja na uwanja wa ndege wa
Mafia (Mafia Airport).
Akizungumza na
vyombo vya Habari mjini hapa, Waziri wa
Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa alisema kuwa “Miradi hiyo yote ya MCC ya kwanza
ilikwenda vizuri sana na tunamaliza nao mkataba tukiwa tumefanikiwa sana katika
ujenzi wa miradi hiyo”.
Aidha Mgimwa
aliendelea kutoa ufafanuzi akisema kuwa “lengo kubwa la kukutana na Uongozi wa
MCC ni kuangalia mafanikio yaliyopatikana katika miradi waliyoianzisha na ni nini
tumejifunza kutoka katika hiyo miradi ili tuepuke matatizo katika miradi mingine
inayofuata”.
Katika majadiliano
hayo ujumbe wa Tanzania ulipata fursa ya kuzungumzia miradi ya MCC ya awamu ya pili ambapo MCC wamekubali kuisaidia
Tanzania kueneza umeme vijijini hasa vijiji vikubwa vinavyozalisha mazao kwa
wingi na vijiji vyenye watu wengi pamoja
na kujenga barabara katika maeneo ya
uzalishaji.
“Hii itakuwa
nafasi ya Tanzania kuweza kusaidia kueneza umeme vijijini ambapo wananchi wetu
watapata nafasi ya kutumia umeme huo katika miradi midogo midogo na vile vile
kwa ajili ya kuhakikisha kuwa miradi ya barabara hasa katika vijiji
vinavyozalisha mazao wanaweza kupokea pembejeo na baada ya kuvuna kuweza
kufikisha mazao yao kwa walaji.” Alifafanua Mgimwa.
Hali ya hewa
ya mjini hapa ni baridi kiasi na manyunyu ya hapa na pale.
Imetolewa
na:
Ingiahedi
Mduma
Msemaji
Mkuu
Wizara
ya Fedha
Washington
D.C
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)