TTCL NA SATA ZAANDAA SEMINA KUJADILI NAMNA YA KUDHIBITI WIZI WA MTANDAO (FRAUD MANAGEMENT, REVENUE ASSURANCE AND NETWORK/CYBER SECURITY) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TTCL NA SATA ZAANDAA SEMINA KUJADILI NAMNA YA KUDHIBITI WIZI WA MTANDAO (FRAUD MANAGEMENT, REVENUE ASSURANCE AND NETWORK/CYBER SECURITY)

 1Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi Tekinolojia na Mawasiliano Profesa Patrick Makungu akifungua semina ya siku tatu inayokutanisha Wataalamu mbalimbali wa TEHAMA kutoka nchi za (SADC) zinazounganishwa na taasisi ya Southern Africa Telecommunications Association. (SATA) ili kujadili namna ya kuzuia Wizi na uhalifu kupitia kwenye mtandao (Fraud Management, Revenue Assurance and Network/Cyber Security) inayofanyika kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam ikishirikisha makampuni ya simu katika nchi za kusini mwa Afrika, Katika semina hiyo kumeripotiwa wizi wa fedha unaofikia asilimia 8% mpaka 13% ikiwa ni pamoja na uhalifu mwingine, Semina hiyo imeandaliwa kwa pamoja na Kampuni ya Simu ya TTCL ikishirikiana na Taasisi ya Southern Africa Telecommunications Association. (SATA)2Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya TTCL Dr. Kamugisha Kazaura akizungumza katika semina hiyo wakati akiwakaribisha washiriki wa semina hiyo inayofanyika kwenye honteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam. 8Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada.7 Jacob Munodawafa Katibu Mkuu wa taasisi ya Southern Africa Telecommunications Association.(SATA) akizungumza katika semina hiyo wakati akizungumzia malengo ya SATA kufanya semina hiyo kwa wadau wake.3Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo leo 4Baadhi ya wakuu wa vitengo wa kampuni ya simu TTCL wakiwa katika semina hiyo 5Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi Tekinolojia na Mawasiliano Profesa Patrick Makungu akiandika baadhi ya mambo muhimu katika semina hiyo kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya TTCL Dr. Kamugisha Kazaura akizungumza 6Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi Tekinolojia na Mawasiliano Profesa Patrick Makungu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-KUNDUCHI

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages