TANGA WAZINDUA MRADI WA KUWAJENGEA UWEZO WASICHANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TANGA WAZINDUA MRADI WA KUWAJENGEA UWEZO WASICHANA

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu na kiongozi wa Taasisi ya Tanga Women Development Initiative (TAWODE) wakizundua  mradi huo.
 Watoto wakike ambao ndio walengwa wa mradi huo wakiwa na vyeti vyao.
 Watoto wa Kike wakifuatilia uzinduzi wa taasisi yao.
 Moja ya vipeperushi
OKTOBA 11 ya kila mwaka ni siku ya mtoto wa kike duniani. Mkoani Tanga waliadhimisha siku hiyo ya mtoto wa kike kwa kuzindua mradi maalum wa kuwajengea uwezo wasichana wa mkoa wa Tanga chini ya Taasisi ya Tanga Women Development Initiative (TAWODE).

Mgeni rasmi katika uzinduzo huo uliofanyika uwanja wa michezo wa Mkwakwani alikuwa Mhe Chiku Galawa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, na kuhudhuriwa pia na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Tanga wakiongozwa na Halima Dendegu .

Akizungumzia uzinduzi huo Naibu Waziri mwenye dhamana hiyo ya Jinsia, Ummy Mwalimu alisema kuwa amefurahishwa sana na uzinduzi wa mradi huo.

“Kupitia mradi huu ninafurahi kuona nikitekeleza kwa vitendo dhamira yangu kama kiongozi - 'niliechaguliwa' na wanawake wa mkoa wa Tanga- kuchangia kuboresha maisha ya Wanawake na Watoto wa Mkoa wa Tanga”, alisema Mwalimu.

Pia shukrani zilienda kwa Balozi wa Denmark nchini, Johnny Flento kwa kuunga mkono jitihada hizo.

Mradi huo utatekelezwa ktk Wilaya za Pangani, Muheza, Mkinga, Lushoto na Tanga Mjini, umelenga kuchochea uwezo na ubora wa wasichana (wa umri wa miaka 10-24), kutambua weledi na umuhimu wao kwa maendeleo yao na ya jamii zao.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa alisema kuwa kupitia mradi huo Mkoa umedhamiria kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wasichana waliopo katika shule za Serikali za Msingi na Sekondari, kuboresha hali ya afya ya uzazi, kupunguza mimba za mapema, ndoa za utotoni na maambukizi ya VVU.

“Tumepanga kuwafikia moja kwa moja wasichana 16,000 na zaidi ya 100,000 kupitia njia mbalimbali ikiwemo mabango, Radio jingles (Mwambao FM 106.0), matamasha ya wasichana na njia nyingine mbalimbali,”alisema Galawa.

Aidha Wasichana 1,000 waliopo shuleni na wanaoishi ktk mazingira magumu wataingizwa katika Mfuko wa Bima ya afya ili kuweza kupata huduma za afya bure.

Endapo jitihada hizo zitazaa matunda zitachochea maendeleo ya wanaTanga ambao wamekuwa na utayari wa kupokea ushauri na mawazo ya wadau mbalimbali  juu ya Utekelezaji mzuri wa Mradi huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages