TAMASHA LA UTAMADUNI KUADHIMISHWA WILAYANI HANDENI-TANGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAMASHA LA UTAMADUNI KUADHIMISHWA WILAYANI HANDENI-TANGA

Mratibu wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, pichani.
…………………………………………………………………………..
Hayo yamesemwa na mratibu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana,
alipozungumza na mwandishi wa mtandao huu mapema leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza mipango ya kuandaa tamasha hilo la aina yake na lenye mguso wa kuwakutanisha wadau wote kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
 
Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo, Mbwana alisema
endapo wadau wote, wakiwamo wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni, taasisi za serikali watashirikiana katika hilo, mambo yatakuwa mazuri.
Alisema hali hiyo inamfanya aone haja ya kuwataka watu hao washirikiane kwa pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha la utamaduni na michezo Handeni linafanyika kwa mafanikio na kuweka historia mpya.
 
“Watu wote wana umuhimu katika kufanikisha kwa tamasha hili,
hivyo kila mmoja kwa nafasi yake tunaomba msaada wake hata wa kimawazo, ukizingatia kuwa kinachofanyika kwa sasa ni kuachiana majukumu tu.
 
“Tunawaomba wote wenye moyo wa kufanikisha wazo hili
tushirikiane nao kwa namna moja ama nyingine, hasa kwa kuona wenye kampuni zao, mashirika na taasisi za serikali pia kutudhamini katika hili,” alisema Mbwana.
 
Kwa mujibu wa Mbwana, kufanyika kwa tamasha hilo kutakuwa ni
sehemu nzuri ya kuwakutanisha wadau, wananchi wa Handeni na Tanzania kwa ujumla kwa ajili ya kujadiliana changamoto zinazowakabili kwa maendeleo yao.
 
Tamasha hilo la Utamaduni linaandaliwa chini ya Raha Company
and Entertainment huku likifanyika kwa mara ya kwanza katika wilaya hiyo
inayoongozwa na Mkuu wake wa Wilaya Muhingo Rweyemamu, wakati mbunge ni Dk Abdallah Omari Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages