Pages

SERENGETI FIESTA YATIKISA JIJI LA MAHABA TANGA USIKU WA KUAMKIA LEO



Shilole na skwadi lake wakilishambulia jukwaa usiku huu.
pichani juu na chini ni Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria,J-Mrtin akitumbuiza jukwaani usiku wa leo,kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,ambaye pia ni mtoto wa Mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini,Mzee Zorro,Maunda Zorro akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga wakati tamasha la Serengeti fiesta 2013 likiendelea.
Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya uwanja wa Mkwakwani
Sehemu ya mashabiki wakishangweka huku manyunyu ya mvua yakisumbua hapa na pale usiku huu.span>
Mkali mwingine wa miondoko ya mitindo huru,God Zilla akishusha mistari yake mbele ya mashabiki wake waliokuwa wakiitikia kwa pamoja,ndani ya uwanja wa mkwakwani usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea,sambamba na hali ya hewa ya mvua mvua huku mashabiki wakiendelea kupiga mayowe na miluzi kila kona ya uwanja.
Mwanadada Linah ambaye anafanya vyema katika ya muziki wa Bongofleva akicheza na shabiki wake jukwaani.
Msanii ambaye ni muigizaji lakini pia anasumbua sana katika anga ya muziki wa bongofleva,Shilole sambamba na skwadi lake wakilishambulia vilivyo jukwaa usiku huu wakati tamasha la serengeto fiesta likiendelea ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
PICHA ZAIDI INGIA LIVE MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)