Pages

Rais Kikwete Azindua na Kukagua Kiwanda Cha Azam

D92A1807
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua moja ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha vinywaji baridi cha Azam wakati Rais alipotembelea na kuzindua uzalishaji katika kiwanda hicho huko Mwandege, Wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani leo. D92A1927Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa waajiriwa wa kiwanda cha Bakhressa Food Products Bi.Khadija Isihaka wakati Rais alipozindua uzalishaji katika kiwanda hicho kilichopo chini ya Kampuni ya Azam huko Mwandege,Wilyani Mkuranga leo.Kiwanda hicho kimetoa ajira kwa zaidi ya watu 400. D92A2030Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi uzalishaji katika kiwanda cha Bakhressa Food Products huko Mwandege, Wilayani Mkuranga  leo asubuhi.Kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Wapili kushoto ni mmiliki wa kiwanda hicho Bwana Said Bakhressa na kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Abdallah Kigoda(picha na Freddy Maro).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)