P-SQUARE KUKANYAGA TENA ARDHI YA TANZANIA MWEZI NOVEMBA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

P-SQUARE KUKANYAGA TENA ARDHI YA TANZANIA MWEZI NOVEMBA



Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela)akizungumza na waandishi  wa habari wakati wa kutangaza ujio wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya  Peter na Paul Okoye maarufu kama P – Square kutoka nchini Nigeria  pamoja na mdhamini Mkuu,Tarehe 23 Mwezi ujao ndipo watawasili nchini.  Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini humo.  Pamoja nae katika Picha ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasilino wa  Vodacom Tanzania Kelvin Twissa ambo ndio wadhamini wa onesho hilo.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasilino wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa,  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza ujio wa wasanii  wa Muziki wa kizazi kipya Peter na Paul Okoye maarufu kama P – square  kutoka nchini Nigeria chini ya udhamini wa Vodacom, watakaowasili Tarehe 23 Mwezi ujao. Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13 kutoka  nchini humo. Pamoja nae katika picha ni Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela).
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa  wazungumzaji Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela).  Na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasilino wa Vodacom Tanzania Kelvin  Twissa , wakati wa Kutangaza ujio wa wasanii wa Muziki wa kizazi kipya  Peter na Paul Okoye maarufu kama P – square kutoka nchini Nigeria,  Tarehe 23 Mwezi ujao. Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13  kutoka nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages