Mratibu
wa taifa wa utepe mweupe wa Uzazi salama Tanzania Mama Rose Mlay
akizungumza katika Mkutano wa siku moja kati ya Uongozi wa Mkoa wa
Rukwa, viongozi wa dini, wabunge, viongozi wa asasi za kijamii na za
kidini na Muungano wa utepe mweupe wa Uzazi wa Salama Tanzania katika
ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga tarehe 8 Oktoba 2013. Akielezea malengo
ya mkutano huo alisema Serikali ya Tanzania inaheshimu ahadi yake ya
kuwa na asilimia hamsini ya vituo vya afya Mkoani Rukwa vitakavyotoa
huduma kamili za dharura za uzazi zikiwa ni pamoja na upasuaji kumtoa
mtoto na kutoa damu salama zinapohitajika ifikapo 2015. Ktikati ni Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla.
Vikundi kazi katika kujadili mpango mkakati utakaotumiwa kuendeleza umuhimu wa huduma za uzazi salama katika jamii.
Dkt. Lunyelele akichangia moja ya mada katika Mkutano huo.
Picha ya pamoja
Chakula cha pamoja. (Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)