MAZISHI YA BABA MZAZI WA MSANII WA KIZAZI KIPYA 20 PERCENT WAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA KIMANZICHANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAZISHI YA BABA MZAZI WA MSANII WA KIZAZI KIPYA 20 PERCENT WAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA KIMANZICHANA

Abas Kinzasa kwa jina la usanii anaitwa 20 Percent akiwa kwenye majonzi baada ya kufiwa na Baba yake mzazi Mzee Kinzasa aliyefariki juzi siku ya Jumapili na kuzikwa siku ya Jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Hapa ndipo alikozikwa Mzee Kinzasa baba mzazi wa 20 Percent aliyefariki siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga

Msanii 20 Percent na ndugu zake wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu baba yake mzazi mzee Kinzasa
Abas Kinzasa kwa jina usanii anaitwa 20 percent akieleza jambo kandokando ya kaburi la  Baba yake mzazi Mzee Kinzasa aliyefariki siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga

Marehemu mzee Kinzasa akiombewa dua baada ya kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele
Hii ndio nyumba aliyoicha marehemu Mzee Kinzasa iliyoko kwenye kijiji cha Kimanzichana
Baadhi ya wananchi waliofika msibani
Wazee wakiesabu kiasi cha pesa kilichopatikana kwa watu waliotoa rambirambi zao kwenye msiba wa marehemu Mzee Kinzasa
Mzee
akieleza jambo kwenye msiba wa baba yake na 20 Percent aliyefariki siku
ya Jumapili na kuzikwa nyumbani kwake kwenye kijiji cha Kimanzichana
Mwenyekiti wa mtaa wa Kimanzichana akimkabidhi mtunza pesa, pesa alizopewa na wananchi kwa ajili ya rambirambi
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye msiba wa baba yake na 20 Percent kwenye
kijiji cha Kimanzichana kilichoko wilaya ya Mkulanga mkoani Pwani hapo jana mchana
Mtunza pesa akieleza kiasi cha pesa zilizopatikana baada ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika msibani hapo  kutoa rambirambi zao. PICHA NA PAMOJA/PAMOJAPURE BLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages