Anashangilia: Nyota wa Bayern Munich, Thomas Muller (kulia) akishangilia bao na wachezaji wake baada ya kuweka ubao wa mabao usomeke 2-0
Hakuna mechi hapa: Frank Ribery (kulia) akikokota mpira mbele ya beki wa kulia wa City,Micah Richards
Staili mpya hii: Arjen Robben wa Muenchen akishangilia bao la tatu na wachezaji wenzake
Katika
mchezo mwingine, kocha David Moyes wa Manchester United alilazimishwa
sare ya 1-1 Shakhtar Donetsk Uwanja wa Donbass Arena.
Danny Welbeck alitangulia kuifungia United dakika ya 18 kabla ya Taison kuwasawazishai wenyeji dakika ya 76.
Shakhtar
Donetsk: Pyatov, Srna, Kucher, Rakitskiy, Shevchuk, Fernando/EeIlsinho
dk84, Hubschman, Taison/Bernard dk90, Alex Teixeira, Douglas Costa na
Luiz Adriano/Ferreyra dk90).
Manchester
United: De Gea, Rafael Da Silva, Smalling, Vidic, Evra, Valencia,
Carrick, Fellaini/Giggs dk66, Cleverley, Welbeck/Jones dk90 na van
Persie.
Mkombozi: Taison akimpeleka sokoni kipa wa Man United, David De Dea na kuisaidia Shakhtar Donetsk
Kazi nzuri: Man United walijikakamua sana kupata sare jana
Historia: Giggs aliingia uwanjani na kumbadili Marouane Fellaini kipindi cha pili na kucheza mechi ya 145
Nao
Real Madrid imeifumua mabao 4-0 FC Copenhagen mawili akifunga Angel Di
Maria na mawili Cristiano Ronaldo, ambaye amesherehekea kucheza mechi ya
100 michuano ya Ulaya.
Ronaldo
ametimiza mabao 212 katika mechi 208 alizocheza Madrid – na sasa
mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United amefunga mabao 40
katika mechi 42 za Ligi ya Mabingwa akiwa Real.
Real
Madrid: Casillas, Carvajal, Pepe, Varane, Marcelo, Di Maria,
Modric/Isco dk67, Khedira/Morata dk74, Illarramendi, Benzema/Jese dk81
na Ronaldo.
FC
Copenhagen: Wiland, Jacobsen, Mellberg, Sigurdsson, Bengtsson, Gislason,
Delaney, Claudemir, Toutouh/Bolanos dk63, Braaten/Adi dk67,
Jorgensen/Kristensen dk72.
Usiku mweupe: Cristiano Ronaldo akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kuweka kimiani ba la kwanza
Katika
mchezo mwingine, Bao la dakika ya mwisho la Umut Bulut limeinusuru
Galatasaray kuzama chini ya kocha wake mpya, Roberto Mancini kwa kupata
sare ya 2-2 mjini Turin mbele ya Juventus.
Didier
Drogba alitangulia kipindi cha kwanza kuifungia timu hiyo ya Uturuki,
lakini Juventus ikasawazisha na kufunga la pili kupitia kwa Arturo Vidal
na Fabio Quagliarella kabla ya Bulut kuiokoa timu yake mwishoni mwa
mchezo.
Juventus: Buffon, Barzagli, Bonucci, Chiellini, Lichtsteiner, Pirlo, Asamoah, Vidal, Pogba, Tevez, Vucinic.
Galatasaray: Muslera, Eboue, Kaya, Chedjou, Riera, Felipe Melo, Inan, Balta, Sneijder, Bruma, Drogba.
Mnyama wa ukweli: Didier Drogba akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Juventus.
MABINGWA wa Ulaya,
Bayern Munich wameonyesha soka ya kiwango cha juu na kuifumua nyumbani
Manchester City mabao 3-1 Uwanja wa Etihad. Yalikuwa mabao ya wachezaji bora duniani Mfaransa
Franck Ribery dakika ya , Mjerumani Thomas Muller dakika ya na Mholanzi
Arjen Robben dakika ya yaliyoizamisha City katika mchezo huo wa Kundi
D.
Makosa ya kipa Joe Hart na walinzi wake yaliigharimu City leo kabla ya Alvaro Negredo kutokea benchi kwenda kufunga bao la kufutia machozi dakika ya – huku beki wa Bayern Jerome Boateng akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Yaya Toure
Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Hart, Richards, Kompany, Nastasic, Clichy, Toure, Fernandinho, Jesus Navas, Aguero, Nasri/Silva dk70 na Dzeko/Negredo dk57.
Bayern
Munich: Neuer, Rafinha, Boateng, Dante, Alaba, Lahm, Robben/Shaqiri
dk78, Schweinsteiger/Kirchhoff dk76, Kroos, Ribery/Gotze dk85
na Muller. Credits: Fullshangwe Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)