MAKAMU WA RAIS DKT.BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA 6 LA KIMATAIFA LA MADAKTARI WANAFUNZI, JIJINI MWANZA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DKT.BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA 6 LA KIMATAIFA LA MADAKTARI WANAFUNZI, JIJINI MWANZA LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Kimataifa la Madktari Wanafunzi, lililofanyika sambamba na Mkutano wa nne wa Chama cha Madaktari Wanafunzi TAnzania (TAMSA) lililofanyika jijini Mwanza leo, Oktoba 6, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Cheti kutoka kwa Mratibu wa Kongamano la Sita la Kimataifa la Madktari Wanafunzi, lililofanyika sambamba na Mkutano wa nne wa Chama cha Madaktari Wanafunzi TAnzania (TAMSA) ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Hubat Kairuki cha Dar es Salaam, Helga Mutasingwa, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Mhe. Makamu katika kufanikisha Kongamano hilo. Makamu alipokea Cheti hicho leo Oktoba 6, 2013 baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Afya, Dkt. Hussein Mwinyi (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Eng. Evarist Ndikilo, wakijumuika kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano hilo. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages