Dakika
ya 36 Mbuyu Twite alirusha mpira mrefu kama ilivyokawaida yake na
Mganda Khamis Kiiza `Diego` alisukumua gozi kambani na kuandika bao la
pili, na alishangilia kwa staili yake ya kucheza sana.
Baada
ya Yanga kupata bao la pili, waliwachanganya Simba zaidi na kucheza
mpira mwingi na kupiga pasi na maringo mengi uwanjani wakijua kazi ni
nyepesi sana katika mchezo wa leo.
Hamisi
Kiiza aliifungia Yanga SC bao la tatu dakika ya 45 akimalizia pasi
nzuri ya Kavumbangu, ambaye alichanja mbugu na kuipasua ngome ya Simba
SC na kubaki na kipa Abbel Dhaira, lakini akaamua kumpa mwenzake amfunge
Mganda mwenzake.
Kipindi
cha pili mambo yalibadilika kabisa ambapo Simba SC waliingia kwa kasi
na kucheza pasi zao fupi fupi na za uhakika na kusawazisha mabao yote
matatu.
Jembe
la Jangwani: Khamis Kiiza ni hatari sana, ukimuachia na kutoweka
mikakati ya kumkaba lazima ulie na leo katupia 2. (PICHA NA BIZ ZUBEIRY)
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC, `Taifa kubwa` wametoka nyuma kwa mabao 3-0 ya kipindi cha kwanza na kupata sare ngumu dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga katika mchezo uliopigwa dimba la Taifa jijini Dar es salaam chini ya mwamuzi Isarel Mujuni Nkongo.
Hadi mapumziko, vijana wa Ernie Brandts, mchezaji wa zamani wa timu ya Taafa ya Uholanzi walikuwa mbele kwa mabao 3-0, huku mashabiki wao wakishangilia na kuwabiga vijembe vya nguvu watani wao wa jadi kwa staili ya chinja chinja.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Mrisho Khalfan Ngassa dakika ya 15 akimalizia mpira wa juu uliochongwa na Mrundi Didier Kabumbagu na kumchanganya mlinda mlango wa Simba SC Abel Dhaira na kudondokea chini kabla ya `Anko` aliyetangaza kuchoma nyuma kama hatawafunga wanasimbazi kuusukumia nyavuni.
Betram
Mombeki dakika ya 54 alifunga bao safi akipokea pasi kutoka kwa Mrundi
Amisi Tambwe na kupiga shuti lililomwacha Ally Mustafa ‘Barthez’
akishangaa bila kuwa na la kufanya.
Baada
ya ya bao hilo, Yanga wakajua Simba wamejifuta machozi kwa bao hilo,
lakini wapi, kwani ndio moto ukawaka zaidi na dakika ya 58 Joseph Owino
aliunganisha kwa kichwa mpira uliochongwa na Ramadhani Singano `Messi na
kuandika bao la pili la kusawazisha`
Bao hilo hakika liliwachanganya Yanga na wachezaji wa timu hiyo wakaanza kulaumiana wenyewe na kipa wao Barthez.
Kusawazisha
kwa mabao hayo mawili, kuliwafanya Simba wapate nguvu zaidi na kutafuta
bao la tatu, huku wakitawala soka kwa dakika nyingi.
Dakika
ya 85, Mpira wa adhabu uliopigwa na Nassor Masoud ‘Chollo’
uliunganishwa kwa kichwa nyavuni na beki Kaze Gilbert kuipatia Simba SC
bao la kusawazisha dakika ya 85.
Simba
walikuja juu na kucheza soka safi kipindi cha pili kuttokana na
mabadiliko yaliyofanywa na kocha Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King
Kibaden’ kuwatoa Abdulhalim Humud na Haroun Chanongo na kuwaingiza Said
Ndemla na William Lucian ‘Gallas’ mapema kipindi cha pili.
Yanga
wameathiriwa zaidi leo kutokana na kujiamini kupita kiasi, hasa baada
ya kutoka kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa mabao 3-0, lakini pia
mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mholanzi, Ernie Brandts kumtoa Hamisi
Kiiza na kumuingiza Simon Msuva wakati wanaongoza 3-2 nayo yalifanya
mambo yasiende safi wa wanajangwani.
Kikosi
cha Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Haruna
Shamte, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Haruna Chanongo/Said
Ndemla dk48, Abdulhalim Humud/William Lucian ‘Gallas’ dk48, Betram
Mombeki/Zahor Pazi dk90, Amisi Tambwe na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Hamisi Kiiza/Simon Msuva dk61 na haruna Niyonzima.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)