Leodger Tenga Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu aliyemaliza muda wake akimkabidhi Mpira Jamal Malinzi Rais Mpya wa
shirikisho hilo mara baada ya kumshinda mpinzani wake aliyekuwa makamu
wa Kwanza wa shirikisho hilo Bw. Athman Nyamlani kwa kura 73 kwenye
uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Water Front jijini Dar es salaam na
kumalizika usiku wa kuamkia leo, Katika uchaguzi huo Mgombea wa umakamu wa rais
Walace Karia amefanikiwa kuwashinda wapinzani wake Imani Madega na
Ramadhan Nassib. Jamal Malinzi Rais Mpya wa
shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF akizungumza na
wajumbe wa kamati ya utendaji mara baada ya kutangazwa mshindi katika
uchaguzi huo usiku wa kuamkia leo , kulia ni Wallace Karia Makamu wa Rais wa TFF Leodger Tenga Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu aliyemaliza muda wake akizungumza na kumpongeza Jamal Malinzi Rais Mpya wa shirikisho Baadhi
ya wafuasi wa Rais Mpya wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF
Bw. Jamal Malinzi wakishangilia na kupongezana mara baada ya kusikia
matokeo ya uchaguzi huo yakionyesha Jamal Malinzi ameshinda. Baadhi
ya wafuasi wa Rais Mpya wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF
Bw. Jamal Malinzi wakishangilia na kupongezana mara baada ya kusikia
matokeo ya uchaguzi huo yakionyesha Jamal Malinzi ameshinda. Mmoja
wa wajumbe wa kamati ya utendaji Bw. Mvela kutoka Iringa hali
ilibadilika kutokana na furaha jambo lililopelekea kupata mshtuko hapa
akisaidiwa kutolewa nje ya ukumbi na wajumbe wenzake. Kutoka
kulia ni Leodger Tenga Rais wa TFF aliyemaliza muda wake mwakilishi wa
FIFA Ashford Mamelodi na Henry Tandau wakiwa katika chumba cha uchaguzi
huo. Jamal Malinzi Rais Mpya wa
shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF akimpongeza makamu
wake wa Rais Bw. Wallace Karia mara baada ya kutangazwa kwa matokeo
hayo. Leodger Tenga Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu aliyemaliza muda wake akimpongeza Jamal Malinzi Rais Mpya wa
shirikisho hilo mara baada ya kumshinda hapa siyo kwamba walikuwa
wanalia bali walikuwa wakipongezana mara baada ya kazi kubwa ya kusaka
ushindi.PICHA NA KUKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE WATER FRONT DAR ES SALAAM
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)