JESHI
la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Steven Julias mkazi wa Jakaranda
kata ya Iyela Jijini Mbeya akituhumiwa kutelekeza familia kwa miezi
mitano bila huduma za msingi ikiwemo chakula na sare za shule.
Kukamatwa
kwa mtuhumiwa huyo kumethibitishwa na mwenyekiti wa dawati la Jinsia
Mkoa wa Mbeya, Mary Gumbo ambaye alisema walimkamata Oktoba 11, mwaka
huu eneo la nyumbani kwake alikokuwa amewatelekeza watoto hao.
Aliongeza
kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa anafanya maandalizi ya kuwatorosha
watoto hao ili kukwepa mkono wa sheria dhidi yake baada ya kusikia
kwenye vyombo vya habari kuwa anatafutwa kukabili kesi iliyombele yake.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti huyo alisema hivi sasa uchunguzi unafanyika ili
kesi iweze kufunguliwa na hatimaye kufikishwa mahakamani ili sheria
iweze kuchukua mkondo wake ili vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto
vikomeshwe.
Wakati
huo huo maisha wanayoishi kwa sasa watoto hao Agustino Steven (8) na
Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi
Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya maisha ya kujipikia bila
huduma za msingi wasamaria wema wameombwa msaada wao wa hali na mali.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema hivi sasa wanaishi kwa misaada
kutoka kwa walimu na baadhi ya watu ambao huwapa unga na maharage na wao
hulazimika kutafuta fedha za kununulia mahitaji mengine kama mafuta ya
kula na taa.
Wametaja
baadhi ya mahitaji yao muhimu kwa sasa kuwa ni pamoja na Sare za shule
kutokana na kuchakaa kwa sare wanazotumia ikiwemo Madaftari,
kalamu,Masweta, Viatu, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupaka, sabuni,
chumvi, mkaa, Unga, Mchele na maharage.
Aidha
imeshauriwa kuwa kutokana na mazingira wanayoishi watoto hao kutokuwa
mazuri kwa utunzaji wa vyakula ambapo nyumba wanayoishi kutokuwa na
mlango vitu hivyo vihifadhiwe Ofisini Kwa Mwalim Mkuu kama vitapatikana.
Kwa yeyote atakayekuwa ameguswa na hali ya watoto hao awasiliane na Mbeya yetu kupitia namba 0754374408
au Bomba fm redio kupitia 0754 490752.
Picha/Habari Na Mbeya yetu Blog
|
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)