Pages

HAFLA YA USIKU WA CHAKULA CHA HISANI ILIYOANDALIWA NA AMREF TANZANIA NA MONTAGE LIMITED INAENDELEA USIKU HUU KATIKA HOTEL YA SERENA

Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Mohamed Gharib Bilal ambaye pia ni mgeni rasmi katika Usiku wa Chakula cha Hisani kilichoandaliwa na AMREF TANZANIA kwa kushirikiana na Kampuni ya Montage kwaajili ya kuchangisha Pesa kwaajili ya Kusomesha Wakunga, hafla hiyo inayoendelea Usiku Huu katika hotel ya Serena
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wawakilishi wa makampuni yaliyodhamini Usiku wa Chakula cha Hisani unaofanyika katika Hoteli ya Serena Usiku huu kwaajili ya kuchangisha ya kusomesha wakunga.Kampeni hii ya AMREF ijulikanayo kama Stand up for Tanzania Mother yenye lengo la kutafuta pesa ya kusomesha wakunga ili kuweza kutoa huduma ya Mama na Mtoto ili kupunguza vifo vya mama na mtoto katika hospitali za Tanzania
Mgeni rasmi ambaye pia ni Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal akiwa na wageni wengine waalikwa Katika Meza yao katika Usiku wa Chakula Cha Hisani ulioandaliwa na AMREF TANZANIA kwa kushirikiana na Montage Limited Kwaajili ya kutafuta pesa ya Kusomesha Wakunga ili kuweza kusaidia kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto Tanzania
Baadhi ya Wake wa Mawaziri waliohudhuria hafla hii ya Usiku wa Chakula Cha Hisani kwaajili ya Kutafuta pesa ya Kusomesha wakunga kwaajili ya Kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto, Hafla iliyoandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited kupitia kampeni yake ya Stand up For Tanzania Mother
Baadhi ya Wadau waliojitokeza katika Hafla ya Usiku wa Chakula cha Usiku kwaajili ya kutafuta pesa ya Kusomesha Wakunga Hapa Tanzania katika Kampeni ya Stand for Tanzania Mothers iliyoandaliwa na AMREF Tanzania kwa Kushirikiana na Montage Limited, Hafla inayoendelea Usiku huu katika Hotel ya Serena...Picha Zaidi Zitakujia hivi Punde kupitia Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)