Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kumpa pole, baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar wiki iliyopita. Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa Tindikali na watu wasiojulikana, Mjini Unguja, Zanzibar alipofika katika Hospitali ya Muhimbili kumpa pole, ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu. Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimuhakikishia Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Zanzibar jinsi wizara yake itakavyopambana kwa kuwakamata wale wote watakaojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutimia kemikali ya tindikali. Dk Nchimbi alifika hospitalini. Dk Nchimbi alifika katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kumpa pole padri huyo ambaye anatarajiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya kupata matibabu zaidi. Hata hivyo, Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikaliPicha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)