Mh. Balozi Batilda S. Burian akiwa katika zoezi la kutolewa damu pamoja na watanzania wengine aliyoambatana nao.
Balozi
wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda S. Burian, leo ameongoza umati wa
Watanzania waishio hapa Nairobi, Kenya, kujitolea damu kwa ajili ya
kuwasaidia waathirika wa tukio la ugaidi lililotokea Tarehe 21 Septemba
2013 jijini Nairobi Kenya, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 62
wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 179 wamejeruhiwa vibaya na wengi
wao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za Aga Khan
University Hospital, Hospitali ya Nairobi ( Nairobi Hospital), na
Hospitali ya MP Shah.Picha Kwa hisani ya Michuzi Blog
Katika
tukio hilo pia Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko, Meneja, Child
Protection, UNICEF ni mmoja wa wale walioathirika na tukio hilo ambapo
alijeruhiwa kwa risasi na magruneti katika miguu yake yote miwili. Hivi
sasa Bwana Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi na
anendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)