UFUNGUZI WA KIKAO CHA SIKU MBILI CHA WADAU WA FILAMU KUHUSU MJADALA WA SERA YA FILAMU. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UFUNGUZI WA KIKAO CHA SIKU MBILI CHA WADAU WA FILAMU KUHUSU MJADALA WA SERA YA FILAMU.

 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo akitoa hotuba kwa niaba ya mgeni rasmi baada ya ufungua rasmi Kikao cha siku mbili cha Wadau wa Filamu kuhusu Mjadala wa Sera ya Filamu ambaye alimwakilisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Elisante Ole Gabriel katika ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Bw. Suleiman Ling’ande akitoa maneno machache kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ole Sante Grabriel katika ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
 Mshauri Mwelekezi Bw. Ernest Omalla (aliyesimama) akitoa maelezo machache kabla kumkaribisha Mshauri Mwelekezi mwenzie Bw. Martin Cuff (kushoto) kwa ajili ya kutoa somo kwa washiriki katika ukumbi wa TCRA leo jijini Dar es Salaam.
 Mshauri Mwelekezi Bw. Ernest Omalla akitoa somo fupi juu ya Kikao cha siku mbili cha Wadau wa Filamu kuhusu Mjadala wa Sera ya Filamu uliofunguliwa jana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi Joyce Fissoo kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Grabriel katika ukumbi wa TCRA  jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo (kulia) akimsomea maelezo muhimu Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kulia) mara baada ya kukamilisha kutoa hotuba fupi ya mgeni rasmi ambaye alimwakilisha. 
 Baadhi ya Washiriki waliohudhuria uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Filamu wakifuatilia somo toka kwa wadau mbalimbali wa TAFF pamoja na Washauri Waelekezi wakati wa uzinduzi Kikao cha siku mbiloi cha Wadau wa Filamu kuhusu Mjadala wa Sera ya Filamu kilichofanyika jana katika ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages