SERENGETI FIESTA YAFANA JIJINI MBEYA LEO WAKAZI WA IRINGA KUFURAHI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SERENGETI FIESTA YAFANA JIJINI MBEYA LEO WAKAZI WA IRINGA KUFURAHI

Wasanii maarufu Chege na Temba, wakiwaimbisha maelfu ya wakazi wakazi wa jijini Mbeya na majirani zake katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini hapo siku ya Ijumaa katika uwanja wa Sokoine. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.
 Msanii Kassimu Mganga,”mkali wa mahaba” akitumbuiza wakazi wa jiji la Mbeya katika tamasha la Serengeti Fiesta jijini humo lililofanyika katika uwanja wa Sokoine. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.
 Msanii maarufu Ommy Dimpoz, akiwaimbisha maelfu ya wakazi wakazi wa jijini Mbeya na majirani zake katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini hapo siku ya Ijumaa katika uwanja wa Sokoine. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.
Msanii maarufu Rich Mavoko, akiwaimbisha wakazi wa jijini Mbeya na majirani zake katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini hapo siku ya Ijumaa katika uwanja wa Sokoine. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.

Maelfu ya wapenda burudani mjini Mbeya walijitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Sokoine jijini humo kushiriki katika Tamasha la Serengeti Fiesta. Tofauti na ilivyotarajiwa, idadi kubwa ya wananchi wa mkoa huo walijitokeza na kuufunika Uwanja wa Sokoine kwa shangwe mwanzo hadi mwisho.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager ambayo ndio bia inayodhamini tamasha hili kubwa, Allan Chonjo alisema ”Mpaka sasa tumepata wawakilishi sita kutoka Mtwara na Linda waliopata nafasi ya wageni maalum (VIP) ambao ni Jovin Manzi, Mary Joseph, Baraka Shaban, Issa Shabani, Benard Boniface”.

 ”Washindi wote kutika mikoani watakaa jukwaa la watu maalumu ambapo wataweza kushuhudia burudani kwa karibu zaidi na watapata nafasi ya kupiga picha na wasanii wakubwa, hivyo tunawaomba wakazi wa Mtwara waendelee kunywa bia ya Serengeti  ili waweze kujishindia bia za bure na hatimaye kushinda nafasi hiyo ya kuja Dar Es Salaam kwa ajili ya Fiesta ya mwisho”. Wateja wanatakiwa kuangalia chini ya kizibo na kuona kama wajishindia bia za bure, kwani kuna bia zaidi ya laki mbilli nchi nzima,  aliongeza Chonjo.

Mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo, Simon Simalenga alikiri kushangazwa na umati mkubwa uliojitokeza ukilinganisha na mikoa mingine ambayo tayari Fiesta imeshapita. “Watu wamekuwa wengi kinyume na matarajio ila tunafurahi wameburudika na burudani iliyodondoshwa”

Katika tamasha hilo msanii Quick rocka mkali wa kurap  ambaye pia ni mwenyeji wa mji huo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwachezesha maelfu ya watu waliokuwapo uwanjani hapo kupitia ngoma zake kali.

Pamoja na mwenyeji huyo wasanii kibao walifanya vizuri akiwamo Ney wa Mitego, Madee, Juma Nature, Shilole, Walter Chilambo, Stamina, Young Killer na Godzilla. Shangwe ziliibuka upya Ney wa  mitego alipopanda stejini na kuimba wimbo ulioimbwa na mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Wengine ni Afande Sele, Ommy Dimpoz, Rich Mavoko, Chege, Temba, Kassim Mganga, Joh Makini na Nick wa Pili. Orodha hiyo hiyo inatarajiwa kutoa burudani siku ya leo  kwa wakazi wa Mji wa Iringa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages