semina ya kamata fursa twendzetu yafanyika mkoani shinyanga leo. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

semina ya kamata fursa twendzetu yafanyika mkoani shinyanga leo.

 
 Mbuge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Wa Nishati na Madini,Mh Steven  Masele akizungumza na sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika  kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo  kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.Mh Steven amewataka vijana wa  Shinyanga kuwa na moyo wa kujituma na kuzifanyia kazi ipasavyo fursa  wanazokumbana nazo bila kukata tamaa,ameeleza kuwa hivu karibuni mkoa  huo,unatarajia kufungua viwanda kadhaa,ambapo anaamini kuanzia fursa ya  kupata ajira kwa vijana itaongezeka.
 Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Maxmalipo,Bernard Munubi akizungumza  kwenye semina ya Kamata Fursa Twendzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala  mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za  jamii,ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.
 sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya  Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga  Vijana Center. 
 Mkurugezi  wa Vipindi na Uzalishaji Kutoka Clouds Media Groug,Ruge Mutahaba akizungumza sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.Ruge pia amefunga semina hiyo ya fursa kwa vijana mapema loe mchana,ambayo imekuwa ikiandaliwa na kampuni ya Clouds Media,Semina hiyo imefanyika  ndani ya mikoa takribani zadi ya kumi  ikiwemo Kigoma,Singida,Tabora,Mtwara,Morogoro,Dodoma,Mbeya, Iringa,Bukoba na sasa ndani ya mkoa wa Shinyanga.
 sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya  Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga  Vijana Center.  
 Wengine tena ndio hivyo teena,fursaaa fursaaaaa. 
 Sehemu ya meza kuu ikifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.
 Wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini.
 Mtangazaji wa Clouds FM,Shaffih Dauda akitoa mada ya fursa ndani ya michezo na changamoto zake,lakini pia namna ya kukabiliana nazo kiasi hata kupata mafanikio kwa namna moja ama nyingine,
Mwakalilishi kutoka TPSF,Jane Gonsalves akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twendzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali ya ujasiliamali kwa vijana ikiwa ni sehemu pia kujiongezea kipato,semina hiyo imefanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Center. 
Baadhi wakazi wa mkoa wa Shinnyanga wakifuatila mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,semina hiyo imefanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.Picha na Michuzijr wa MICHUZI MEDIA GROUP-SHINYANGA.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages