OFISI YA TTB KANDA YA ZIWA MWANZA YAZINDULIWA RASMI NAIBU WAZIRI, ASEMA TATIZO LA BAJETI FINYU KWA TTB LITAPATIWA UFUMBUZI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

OFISI YA TTB KANDA YA ZIWA MWANZA YAZINDULIWA RASMI NAIBU WAZIRI, ASEMA TATIZO LA BAJETI FINYU KWA TTB LITAPATIWA UFUMBUZI

Photo 1Ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kanda ya ziwa iliyoko katika jingo la hotel ya Mwanza muda mfupi kabla ya kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (MB). Photo 2Kikundi changoma kutoka kituo cha utamaduni cha Bujora mkoani Mwanza kikitoa Burudani ya ngoma ya kucheza na chatu mbele ya ofisi ya Bodi ya Utalii kanda ya ziwa jijini Mwanza mara ru baadaya mgeni rasmi Naibu Waziri Lazaro Nyalandu kuwasili ofisini hapo ili kuizindua ofisi hiyo. Photo 3Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazro Nyalandu (MB) akizungumza na wandishi wa habari ndani ya ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania – TTB kanda ya ziwa jijini Mwanza muda mfupi baadaya kuizindua . Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr. Aloyce Nzuki.
……………………………………………………….
 Na Geofrey Tengeneza, Mwanza
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (MB) ameiambia  ya Bodi ya Utalii Tanzania – TTB kuwa tatizo la sugu bajeti isiyotosheleza mahitaji ya Bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yake litapatiwa ufumbuzi kwa kiasi kikubwa mara baada ya fedha kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya Utalii (Tourism Development Levy kuanza) kuanza rasmi ambapo moja ya vyanzo vyake vya  fedha  ni tozo la kitanda siku kwa watalii watakaokuwa wakilala katika hoteli mbalimbali.
 
Mheshimiwa Nyalandu ameyasema hayo wakati akizindua ofisi ya Bodi ya Utalii kanda ya ziwa iliyoko jijini Mwanza. Amesema Bodi ya Utalii inapaswa kutengewa bajeti ya kutosha kuiwezesha kumudu ushindani uliopo wa kutangaza vivutio vyetu katika masoko ya watalii na kuvutia watalii wengi. “ Tuiwezeshe kwanza TTB kwa kuipa fedha za kutosha kutekeleza majukumu yake ndipo tuwaluamu wakishindwa” alisema. Kuzinduliwa kwa ofisi ya TTB mkoani Mwanza  ambako kumefanyika sambamba na maadhimisho ya siku ya Utalii duniani ni jitihada za Bodi ya Utalii Tanzania kusogeza huduma zake zaidi kwa wananchi ambapo ofisi hii ya Mwanza ni ya tatu, baada ile ya Kanda ya Kaskazini na ile ya Kanda ya nyanda za juu Kusini iliyoko mjini Iringa. Ofisi hii ilianza kazi jijini Mwanza tangu Novemba 11, 2011 ambapo awali ilianzia katika eneo la Kapripointi kabla ya kuhamia katika jengo la hoteli ya Mwanza (Mwanza Hotel) katikati ya jiji hili la Mwanza Desemba 27, 2012. 

Tangu kufunguliwa na kuanza kutoa huduma mkoani Mwanza ofisi hii ya bodi ya Utalii imepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wageni hususan wa nje wanaotembele ofisi hii ili kupata taarifa ya vivutio vya utalii vilivyopo hapa Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla. Kwa mfano kuanzia Desemba 26, 2012 hadi Machi 2013 idadi ya wageni waliotembelea ofisi yetu  walikuwa 102; kuanzia Aprili hadi June 2013 walikuwa 97; na kuanzia Julai hadi tarehe 27/9/2013 ofisi hii ilopozinduliwa rasmi idadi ya wageni imefikia 242. Hivyo jumla ya wageni (watalii) kutoka nje ya nchi waliotembelea na kupata taarifa za utalii katika ofisi yetu toka imefunguliwa ni 441.

Mafanikio mengine ni pamoja na Bodi ya Utalii kupitia kitengo chake cha Utalii wa Utamaduni (Cultural Tourism Program) kwa kushirikiana na ofisi hii ya Kanda kuanza kutoa huduma za ushauri wa kuendesha kuiutaalamu zaidi shughuli za Kikundi cha Utalii wa Kitamaduni cha Kisesa (Kisesa Eco & Cultural Tourism). Tunatambua na kushirikiana na Kituo cha Kumbukumbu cha Kabila la Wasukuma cha Bujora na ambacho tumekuwa tukikitangaza kwa muda mrefu sasa kama moja ya vivutio vilivyoko hapa Mwanza. Aidha ofisi yetu hii ya Kanda hapa Mwanza mpaka sasa imeweza kutoa nafasi ya mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi sita kutoka vyuo mbalimbali kikiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino-SAUT. Aidha kupitia ofisi ya Kanda Bodi ya Utalii Mwezi Februari ilileta mkoani Mwanza wandishi wa habari wa kimataifa wawili kutoka Uturuki ili kuandika na kupiga picha vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Mwanza kwa lengo la kuvitangaza katika nchi hiyo

Kufunguliwa kwa ofisi hii ya Kanda kutasaidia kwa kiasi kikubwa sana katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya hapa Mwanza na Kanda ya ziwa na itakuwa ni chachu ya maendeleo ya sekta ya utalii mkoani Mwanza na katika Kanda ya ziwa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages