Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
LIGI
kuu soka Tanzania bara imeendelea kutimua vumbi leo, huku mechi
iliyokuwa na mvuto zaidi kutokana na matokeo ya mechi za nyuma na urejeo
wa Ngassa baina ya mabingwa watetezi, klabu ya Yanga dhidi ya Ruvu
Shooting ikimalizika kwa wanajangwani kuibuka kededea kwa bao 1-0.
Bao
hilo pekee limefungwa katika dakika ya 63 kupitia kwa Mganda, Hamis
Friday Kiiza aliyeunganisha krosi murua iliyochongwa na winga machachari
aliyekosa mechi 6 za mwanzo kutokana na kifungo, Mrisho Halfan Ngassa
ambaye alipokea pasi ndefu kutoka kwa kiungo mahiri, Athmani Idd
`Chuji`.
Nimekuja kuchinja: Hamisi Friday Kiiza leo ametumia vizuri kazi nzuri ya Ngassa. Ngassa
mwenye mapenzi makubwa na Yanga imekuwa kama neema kwake kwani tangu
ligi ianze hajawahi kuitumikia timu yake na leo hii amecheza baada ya
jana jioni kulipa deni la milioni 45 alilokuwa akidaiwa na Simba SC.
Kikosi
cha Yanga SC: Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo/Athumani Iddi ‘Chuji’,
Simon Msuva/Nizar Khalfan, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu, Hamisi
Kiiza na Mrisho Ngassa.
Kikosi cha Ruvu Shooting: Abdul Seif, Michael Pius, Stefano Mwasyika, George Michael, Shaaban Suzan, Gedion David, Ayoub Kitala/Said Madega, Hassan Dilunga, Cossmas Lewis, Elias Maguri na Reuben Lambele/Kulwa Mfaume.
Kikosi cha Ruvu Shooting: Abdul Seif, Michael Pius, Stefano Mwasyika, George Michael, Shaaban Suzan, Gedion David, Ayoub Kitala/Said Madega, Hassan Dilunga, Cossmas Lewis, Elias Maguri na Reuben Lambele/Kulwa Mfaume.
Mechi
nyingine iliyokuwa na mvuti wa aina yake kutokana na ubora wa timu hizo
kwa sasa, ilikuwa baina ya Mbeya City waliokuwa uwanja wao wa nyumbani
wa Sokoine kukabiliana na Coastal Union kutoka jijini Tanga.
Mechi
hiyo imemalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 ambapo Coastal walikuwa
wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 7 kupitia kwa Haruna Moshi
`Boban`, lakini dakika ya 70 Mbeya City walisawazisha bao hilo kupitia
kwa mtaalamu wa kupiga ndosi, Mwagane Yeya.
Katika
mchezo huo Coastal Union walianza kucheza soka la Uhakika kipindi cha
kwanza na kudhibiti zaidi eneo la kiungo ambapo Mkenya Jerry Santo,
Abdi Banda, na Haruna Moshi `Boban` waliwatawala viungo wa Mbeya City
wakiongozwa na Antony Matogolo, Steven Mazanda na Deus Kaseke.
Licha
ya Coastal kucheza kwa ufundi, City walionesha ukomavu mkubwa huku
Kaseke akihaha huku na huku kuwaletea shida kubwa mabeki wa Coastal
walioongozwa na Mbwana Hamis, Othman Tamimu, Juma Nyoso na Marcus
Ndeheli.
City
walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini wachezaji wake, Paul Nonga,
Deus Kaseke walishindwa kuzitumia na kubadili kuwa mabao.
Mchezo
huo ulitawaliwa na ubabe kiasi Fulani na katika dakika ya 89, Richard
Peter wa City na Marcus Ndeheli wa Coastal walioneshwa kadi nyekundu
baada ya kuzozana mbele ya mwamuzi wa kati Odern Mbaga kutoka Dar es
salaam.
Dakika
4 baadaye, Haruna Moshi alioneshwa kadi nyekundu baada ya kutumia lugha
mbaya kwa mwamuzi msaidizi na Mbaga kufanya kazi yake. Baada
ya mchezo huo, Kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi hakutaka kuongea na
waandishi wa habari, lakini alitamka jambo moja tu kuwa mpira umekwisha,
wamepata sare, hakuna linginei.
Kwa
upande wa kocha wa Coastal Union, Hemed Morocco alisema mechi ilikuwa
nzuri, walipanga kushinda lakini mipango yao imeshindwa kutimia, hivyo
wanajiandaa na mchezo mwingine. Akiizungumzia
Mbeya City, Morocco alisema ni timu nzuri, ina wachezaji waliofiti
dakika zote na wanajua kujipanga, lakini akatahdharisha kuwa inatakiwa
kupewa muda na wasilazimishe kufika mbali kwani wakati wake utafika tu.
Pia
aliwatupia lawama waamuzi kuwa wanatakiwa kukaa chini na kuwa na utu
kwani nao wachezaji ni binadamu kama walivyo wengine, hivyo si kila
wanapokosea wanatakiwa kupewa adhabu kubwa kama ilivyokuwa leo.
Niacheni
nikapumzike jamani: Mlinda Mlango wa Coastal Union, Shaban Hassan Kado
alitoka dakika za mwisho za kipindi cha kwanza baada ya kupata majeruhi.
(Picha na Rashid Mkwinda)
Mbeya
City: David Burhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius,
Yohana Morris, Antony Matogolo, Alex Seth, Steven Mazanda, Paul Nonga,
Deus Kaseke, Francis Casto.
Wachezaji wa akiba: Geofrey Jackson, Baraka Haule, Yusuph Willson, Peter Mapunda, Richard Brown, Mwagane Yeya, Richard Peter.
Coastal
Union: Shaban Kado, Mbwana Hamis, Othman Tamimu, Juma Nyoso, Marcus
Ndeheli, Jerry Santo, Uhuru Seleman, Abdi Banda, Pius Kisambale, Haruna
Moshi, Crispine Odula.
Wachezaji wa Akiba: Said Lubanda, Hamad Hamis, Yusuph Chuma, Razak Halfan, Yayo Lutimba, Keneth Masumbuko, Daniel Lyanga. Mechi
nyingine ya ligi hiyo iliwakutanisha Rhino Rangers katika dimba lao la
A.H. Mwinyi dhidi ya Kagera Sugar na mchezo huo umemalizika kwa
wanajeshi hao wa jeshi la wananchi la Tanzania, (JWTZ) kulala bao 1-0.
Bao hilo pekee kwa wakata miwa wa Kaitaba limefungwa na Themi Ferlix
katika dakika ya 66.
Ligi
hiyo itaendelea kesho ambapo JKT Ruvu watakuwa katika uwanja wao wa
nyumbani wa Taifa jijini Dar es salaam kuvaana na Simba, Ashanti United
watakuwa na kibarua mbele ya Mtibwa Sugar uwanja wa Azam Complex, wakati
huo huo Tanzania Prisons watakuwa Sokoine kula sahani moja na Azam fc.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)