Mtanzania mmoja, Vedasto Nsanzugwanko ambaye alijeruhiwa
kwenye shambulio la Kenya akiwa hospitali
---
Wakati wa Jeshi la Polisi la Tanzania likisema
linafuatilia taarifa za vitisho za kundi la Al-Shabaab la Somalia za
kushambulia, Mtanzania mmoja, Vedasto Nsanzugwanko ambaye alijeruhiwa
kwenye shambulio la Kenya ameelezea yaliyomkuta.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),
Robert Manumba alisema jana kuwa wameanza kufuatilia kwa undani taarifa
zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kwamba kundi la Al-Shabaab
linajipanga kuishambulia Tanzania na Uganda.
DCI Manumba alikiri kusikia taarifa hizo na kusema
kuwa Jeshi la Polisi limeanza kufanya uchunguzi wa kina: “Siwezi
kukueleza ni uchunguzi wa aina gani tutakaofanya, hiyo ni siri yetu.”
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ),
Meja Eric Komba alisema kuwa kuna uwezekano taarifa hizo zikapikwa na
wajanja wachache kwa ajili ya kuwajengea hofu wananchi.Kwa habari zaidi bofya na Endelea.......
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)