MOYES ANAHAITAJI MSAADA, AJUTIA KUSHINDWA KUSAJILI MAJIRA YA KIANGAZI…AHOFIA KIPIGO CHA JUMAPILI KUTOKEA TENA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MOYES ANAHAITAJI MSAADA, AJUTIA KUSHINDWA KUSAJILI MAJIRA YA KIANGAZI…AHOFIA KIPIGO CHA JUMAPILI KUTOKEA TENA

Hang your head: David Moyes has had plenty to think about since Sunday's 4-1 loss to Manchester CityKichwa chamgonga kweli: David Moyes bado amechanganyikiwa na kipigo cha 4-1 jumapili kutoka kwa wanaume wa kazi Manchester City 
 
Klabu ya Man United ilishindwa kumsajili Thiago Alcantara na Cesc Fabregas kutoka FC Barcelona, wakati huo huo nyota wa Real Madrid, Mesut Ozil aliyekuwa akiwindwa pia alijiunga na Arsenal kwa dau lililovunja rekodi ya klabu hiyo la pauni milioni 42.5.

Alipoulizwa kama anahitaji wachezaji zaidi, Moyes alisema: ‘Ni kweli tunahitaji kuleta wachezaji wapya, sio kwenye kikosi moja kwa moja, lakini ni kuangalia kwanza. Nadhani hili litatekelezwa” “Tunaelekea dirisha dogo la usajili, mara zote tunasema tutapambana kutafuta wachezaji na tutatuma ofa nyingi zaidi na zaidi. Kiukweli nahitaji kupata wachezaji wawili zaidi”.
Ouch: Moyes was outthought by Manuel Pellegrini, and admits that that could happen more often this seasonDuuh! kali kweli: Hofu ya Moyes inazidi kushika kasi baada ya kutunguliwa mabao 4-1 na Manuel Pellegrini, na amekiri kuwa kipigo kama hicho kinaweza kutokea kweli
Major signing: The Scot reuinited with former Everton colleague Marouane Fellaini in a disappointing summerUsajili mkubwa: Mscotishi aliungana tena na kiungo wake wa zamani akiwa Everton Marouane Fellaini katika majira ya kiangazi na mabaya kwake

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.

KOCHA wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini England, Manchester United, David Moyes amesema yuko tayari kuivaa Liverpool leo katika kombe la Capital One, lakini amekiri kuwa anahitaji wachezaji wapya wawili ili kushinda mataji.

Moyes amesema amekubali kukosolewa kwake baada ya kipigo cha jumapili ya wiki iliyopita cha mabao 4-1 katika mechi ya watani wa jadi, Manchester United dhidi ya Manchester City.

Lakini kukosolewa kwa Moyes kulianza hata kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu, hasa baada ya kushindwa kuwashawishi wachezaji wengi kujiunga na United katika dirisha la majira ya kiangazi.
 
Kocha huyo wa zamani wa Everton amekutana na wakati mgumu katika mechi ya kwanza ya watani wa jadi ” Manchester derby”, kitu ambacho ni tofauti na kocha mwenzake ambaye ni mpya pia Manuel Pellegrini.
 
City walisajili wachezaji wengi kuliko United majira ya kiangazi, na kuondoka kwa kocha aliyekuwa na ushawishi mkubwa, Alex Ferguson, Moyes amesema kuwa kikosi chake kwa sasa kipo kipindi cha mpito.
Aliongeza “Tuna siku kama ya jumapili na lazima zitatokea zaidi kwa wakati huu wa mpito”

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages