Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa CHADEMA jimbo la Maswa Magharibi Mh. John Shibuda wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Meatu mjini Meatu, ambapo ameelezea kuwa Siasa siyo ugonvi na alikuja Meatu kwa sababu mbili tu Moja ilikuwa ni kukutana na Ndugu Kinana kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali juu ya tatizo la zao la Pamba kuhusu bei ya zao hilo na matatizo ya pembejeo kwa wakulima wa Wilaya hiyo, Akongeza kwamba jambo lia pili ni kwamna Ndugu Abdulrahman Kinana ni rafiki yake wa muda mrefu kwa hata wakati wakisoma shule wote walisoma moshi Abdulrahman Kinana akisoma Old Moshi Sekondari na John Shibuda Mwenyewe akisoma Moshi Technical lakini pia akasema wakati alipokuwa akigombea ubunge wa Maswa Magharibi Kinana alimchangia shilingi Milioni moja "Siasa nia Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana kwa hoja" amemaliza Shibuda. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo katika mkutano huo huku Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi John Shibuda akimsiliza, kushoto anayetabasam ni Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye. Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano huo kushoto ni John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA. Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akikumbatiana kwa furaha na John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA mara baada ya kupanda jukwaani katika viwanja vya Meatu mjini, kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuhudia. Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA Mh John Shibuda akiwasili katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Meatu mjini Meatu leo huku vijana wa Chama chaCHADEMA wakimsindikiza.. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wana Meatu katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mjini Meatu. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu8 Abdulrahman Kinana akielekea jukwaani mara baada ya kusimikwa Chifu Kilabanya wa wasukuma wa Meatu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipunga usinga juu mara baada ya kusimikwa Chifu Kilabanya wa Wasukuma wa Meatu katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Meatu. kulia ni Mayanga Kidoyayi Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti (Chifu Kishosha) kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dr Titus Kamani, Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM na Fale Miungumale. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimikwa na Mzee Fale na mama Kwimba Tobongo katika kutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Meatu leo jioni aliyeshika kipaza sauti ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM na kushoto ni Dr Titusi Kamani mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa mgolole mweusi kama ishara ya kusimikwa kuwa chifu Kilabanya wa wasukuma wa Meatu. Mlemavu Daud Deus akikabidhiwa baiskeli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kutano wa hadhara uliofanyika mjini Meatu Simiyu leo Baiskeli hiyo imetolewa na Salim mmoja wa wana CCM wa Meatu. Daud Deus akijaribu kuendesha baiskeli yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na wanaMeatu katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Meatu leo mkoani Simiyu.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MEATU SIMIYU)
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)