Mbilimbi
ni tunda linalotumika kama chachandu (kiungo cha mboga) kwa ajili ya
kuongeza ladha ya chakula, lina uwingi wa asidi (citric acid) ambayo ni
muhimu kwa binadam mahususi kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula mwilini.
Linatumiwa hasa mikoa ya ukanda wa Pwani ikiwemo Dar es Salaam,
Morogoro,Pwani, Lindi na Tanga. Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala
kutoka mkoani Morogoro (imewakilishwa na Irene Maigwa na Betha Shao
wote kidato cha sita) kwenye banda lao la maonesho ya Wanasayansi
Vijana wa Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo
jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi
wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Liberata Kasekwa (kushoto)
akimulezea mwl. Salome Mbago kutoka shule ya sekondari Morogoro
(katikati) aliyeshikilia chupa nyenye dawa ya kuulia wadudu
iliyotengenezwa kwa kutumia limao kwenye maonesho ya Wanasayansi Vijana
wa Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini
Dar es Salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO)
-





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)