David
Moyes ameshindwa kupata ushindi wa kwanza Anfield kufuatia kushindwa
kushinda katika mechi 12 alizocheza katika dimba hilo akiwa na klabu
yake ya zamani ya Everton.
Hali
ni mbaya zaidi kwa Moyes, kwani Wayne Rooney atakaa nje ya dimba kwa
wiki chache zijazo kutokana na kuumia kichwa katika mazoezi ya jana, na
dirisha la usajili linafungwa kesho usiku na Moyes bado anahitaji
kusajili kwa mara ya kwanza.
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
BAO
la Daniel Sturridge katika dakika ya mapema ya 4 limetosha kuwanyanyua
wekundu wa Anfeild, Liverpool katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya
mabingwa watetezi, Mashetani wekundu, Manchester United na kuanza ligi
kuu soka nchini England kwa ushindi wa asilimia 100.
Kikosi
cha Liverpool leo: Mignolet 6; Johnson 6 (Wisdom 78, 5), Agger 7,
Skrtel 7, Enrique 6; Henderson 7, Lucas 6, Gerrard 7; Aspas 6 (Sterling
60, 6), Sturridge 7, Coutinho 8 (Alberto 84).
Wachezaji wa akiba: Jones, Ibe, Kelly, Flanagan.
Mfungaji wa bao: Sturridge 4
Aliyeoneshwa kadi: Aspas
Kikosi
cha Man United: De Gea 6; Jones 5 (Valencia 37, 6), Ferdinand 7, Vidic
6, Evra 6; Carrick 5, Cleverley 7; Young 5 (Nani 62, 6), Welbeck 6,
Giggs 6 (Hernandez 75); Van Persie 5.
Wachezaji wa Akiba: Anderson, Smalling, Lindegaard, Buttner.
Walioneshwa kadi za njano: Cleverley, Van Persie, Carrick, YoungManagers:
Mwamuzi: Andre Marriner 7
Mshabiki: 44,411
Mchezaji bora wa mechi: Philippe Coutinho
Siku
ya leo ni mbaya sana kwa kocha wa Manchester United, David Moyes ambaye
anatetea taji ambalo kocha mstaafu wa klabu hiyo, Sir Alex Ferguson
alitwaa msimu uliopita.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)