Huu ndiyo uhalisia wa maisha Mtoto huyu ambaye hakufahamika jina lake akiwa amembeba mdogo wake huku akiwa amemshika mkono mwingine katika moja ya vijiji tulivyopitia katika ziara ya leo wilayani Itilima.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipita mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kanadi Wilayani Itilima.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Kanadi huku akiongozwa na mkuu wa shule hiyo Mwalimu Samuel George.
Hili ni jengo la zahanati ya kijiji cha Nangale kata ya Ndololezi Kinana alikaguikagua pia
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na mganga mkuu wa Zahanati ya Nangale Dk. Kerenge Nyawawa wakati alipotembelea na kukagua jengo la zahanati hiyo.
Mwenyekiti wa kikundi cha wafanyabiashara wa mazao katika kata kijiji cha Mwanihunda Kata ya migato Bw, Michael Ntulugwa akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokagua ghala hilo la kuhifadhia chakula lililojengwa kwa msaada wa World Vision.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akiwa amekaa kwenye kigoda wakati alipofika kwenye shina namba 15 Shuleni Kata ya Migato, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana watatu kutoka kushoto aliyekaa akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu Ndugu Pascal Mabiti wakati alipokuwa akiongeza na wananchi katika kata ya Migato
Wana CCM wa kata ya Migato wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati akizungumza nao katika shina namba 15 shuleni kata ya Migato.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Mwenyekiti wa wa shina namba 15 Bwana Michael Sama wakati akiwa katika shina hilo kwa ajili ya kuzungumza na wanachama wa shina hilo leo. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea Fedha Taslimu shuilingi 400.000 kutoka kwa Daud Njalu Silanga Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyu wakati alipochangia SACCOS ya Shina namba 15 shuleni Kata ya Migato.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa maji kwa kikombe cha kiasili cha kabila la kisukuma mara baada ya kusimikwa chifu Machibora Kinana
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana mwenye mgolole mweusi akijumuika pamoja na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi kulia wakishiriki kula chakula cha asili ya kisukuma kinachoitwa Michembe, kutoka kushoto ni mkuu wa mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akihoji jambo kwa Afisa Elimu Wilaya ya Itilima Ndugu Rogers Shimwelekwa wakati alipotembeleaujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya ya Itilima leo, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Dk Leonard Masale na wa pili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga lipu pamoja na mafundi wakati alipotembelea ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Itilima leo
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika eneo la Halmashauri hiyo.
Ndugu Nape Nnauye akipanda mti katika eneo la halmashauri ya Itilima
Mkutano wa ndani ukiendelea chini ya mti.
Ndugu Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Gangabilili ambayo ndiyo makao makuu ya Wilaya ya Itilima
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanaakihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Gangabilili makao makuuu ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-ITILIMA SIMIYU
-





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)