KANALI ABDULRAHMAN KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI SHINYANGA JANA,LEO KUANZA MKOA MPYA WA SIMIYU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

KANALI ABDULRAHMAN KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI SHINYANGA JANA,LEO KUANZA MKOA MPYA WA SIMIYU

1Mwekezaji wa viwanda wa vya nguo vya kusindika Pamba na kusokota nyuzi vya Danong Textile Bi. Jing Lin akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa nne kutoka kulia kabla ya kukagua ujenzi wa viwanda hivyo katika ziara yake ya kuimarisha chama na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya chama hicho, Kinana amehitimisha ziara yake leo mjini Shinyanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycommjini humo kesho ataenelea na ziara yake katika mkoa mpya wa Simiyu,  4Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiingia katika eneo la viwanda vya Danong Textile wakati alipokagua ujenzi wa viwanda hivyo jana 5Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lu Yuoqing akimuelezea jambo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akikagua ujenzi wa viwanda hivyo leo, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. 6Haya ni Maboksi yaliyohifadhi mashine mbalimbali zitakazofungwa katika viwanda hivyo mjini Shinyanga. 7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka katika moja ya mashine za kunyanyulia mizigo katika kiwanda hicho kushoto ni Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lu Youqing. 9Baadhi ya wenyeviti wa mashina na matawi katika manispaa ya Shinyanga. 10Baadhi ya wenyeviti wa mashina na matawi katika manispaa ya Shinyanga waliohudhuria katika kutano huo. 11Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia mikono wenyeviti wa matawi na mashina wakati alipowasili kwenye wanja wa Kambarage ambako mkutano wa ndani ulifanyika jana. 12Baadhi ya wana CCM wakiwa katika mkutano huo 13Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lu Youqing akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga leo kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na kushoto Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana 15Wananchi wakiwa awamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara mjini Shinyanga leo. 16Mbunge wa Viti Maalum kupitia mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akiwahutubia wananchi katika mkutano huo kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana 17Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano huo. 19Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Steven Masele akikabidhi matofali elfu kumi na mifuko mia moja ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika moja ya kata za manispaa ya Shinyanga. 20Timu ya Stend FC ambao ni mabingwa wa ligi ya Daraja la Kwanza wakikabidhi vikombe vyao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana. 21Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akitangaza neema ya umeme vijijini kwa wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga. 22Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Steven Masele na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja wakiwasha Pikipiki kama ishara ya kuzizindua kwa ajili ya kukabidhi kwa watendaji wa chama cha mapinduzi katika ofisi za Chama za Kata mbalimbali, Pikipiki hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Steven Masele mbele ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana. 23Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiendesha Baiskeli wakati alipokuwa akiondoka kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara jana jioni. 24Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha Baiskeli wakati alipokuwa akiondoka kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara jana jioni.25Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga jana.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-SHINYANGA)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages