JWTZ LAKANUSHA TAARIFA ZILIZOENEA MITANDAONI KUHUSU WANAJESHI WAKE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JWTZ LAKANUSHA TAARIFA ZILIZOENEA MITANDAONI KUHUSU WANAJESHI WAKE

 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepata habari kupitia mtandao wa Jamii Forum na Gumzo la Jiji  na mingineyo kuwa likizo zimesitishwa Jeshini  na waliokuwa  likizo wameitwa kurudi kazini.
Taarifa hizo pia zimeeleza kwamba Brigedi za Tembo na Kifaru zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kusonga mbele.

JWTZ  linapenda kuwaeleza wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji mtupu na hazina ukweli wowote.  Aidha, taarifa hizo ni zenye nia ya kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu (Tanzania) na majirani zake. 

Sambamba na taarifa hii, pia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa za kutohusika na viunganishi vya JWTZ kwenye mitandao ya  ‘Facebook‘ – (Facebook/JWTZ) na  ‘Twitter‘  (Twitter/ JWTZ).

Mitandao hiyo yenye viunganishi vya JWTZ imekuwa ikijihusisha na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichangiwa na watu mbalimbali, ambapo baadhi yao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji  na zisizo sahihi.  Tunapenda kutaarifu kwamba akaunti za facebook na twitter zilizotajwa siyo za JWTZ.

Hatua zimechukuliwa za kuwatambua wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.

Aidha inasisitizwa kwamba JWTZ lina taratibu za zake zinazotumika kufanya mawasiliano na Vyombo vya Habari, Taasisi, au mtu binafsi kuhusu utoaji wa taarifa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages