CHIKAMBI KARUGENDO RUMISHA ATEULIWA KUWA MSEMAJI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

CHIKAMBI KARUGENDO RUMISHA ATEULIWA KUWA MSEMAJI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

HGCU
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. M.K.Tarishi amemteua Bw. Chikambi Karugendo Rumisha (57) kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Katibu Mkuu amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 6 (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 2003.
Bw. Rumisha ameitumikiwa Wizara tangu mwaka 1984 katika idara mbalimbali hali inayompa uzoefu na uelewa mkubwa wa masuala mbalimbali yanayohusu Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Rumisha alikuwa akitumikia Wizara ya Maliasili na Utalii katika Idara ya Sera na Mipango.

Bw. Chikambi Rumisha ambaye ni mtaalam wa elimu viumbe alihitimu Shahada ya Sayansi – Ekolojia ya Bahari na Wanyama katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1984.  

Ahitimu masomo ya Uzamili katika fani ya Uvuvi na Viumbe wa Bahari  Mwaka 1987 katika Chuo Kikuu cha Bergen, Norway. Amehudhuria Mafunzo mbalimbali ya muda mfupi ndani na nje ya nchi katika masuala ya mipango, utawala, fedha; ufuatiliaji na upelembaji, Mawailiano, na usimamizi wa miradi.

Bw. Rumisha ameitumikia Serikali katika vituo mbalimbali, pamoja na Makao Makuu ya Wizara idara ya Uvuvi alipohudumu kama Afisa Uvuvi, Kilichokuwa Chuo cha Uvuvi Nyegezi- Mwanza alipohudumu kama mkufunzi, Marine Parks alipohudumu Kama Meneja na Mwazilishi wa Taasisi hiyo na  Makao Makuu ya Wizara -Idara ya Sera na Mipango kitengo cha Ufuatiliaji  

Uteuzi huu wa Bw. C.K.Rumisha unafuatia kustafu kwa aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino ya Serikali wa Wizara, Bw. George Matiko kustaafu tangu tarehe 15/06/2013.

Bw. Chikambi K Rumisha uteuzi wake unanzia tarehe 15/8/2013 na utadumu hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
Katibu Mkuu
Wizara ya Maliasili na Utalii

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages