BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU YAFANYA KIKAO NA MAAFISA MIKOPO NA VYUO VYA ELIMU YA JUU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU YAFANYA KIKAO NA MAAFISA MIKOPO NA VYUO VYA ELIMU YA JUU


Mkurugenzi wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sylvia Temu akifungua kikao cha Pamoja kati ya Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na ,Maafisa wa Mikopo kutoka vyuo vya Elimu ya Juu nchini, katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Pearl-Ubungo, Dar Es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo Bw. Onesmus Laizer, akiwasilisha mada katika kikao hicho.


Afisa Mikopo wa Taasisi ya Elimu Ya Watu wazima, Bw. Beny Mwenda akichangia katika kikao kazi kati ya Maofisa Mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bi.Sophia Nchimbi, akiuliza swali katika kikao hicho.

Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU), akichangia mada katika Kikao hicho.

Picha ya Pamoja kati ya Maafisa Mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo, Aliyekaa katikati ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu,Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof .Sylvia Temu, na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Bw. George Nyatega.


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imefanya kikao kazi na maafisa Mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo- Dar Es Salaam na kuazimia kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuboresha shughuli za utoaji mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Kikao hicho kilikuwa kwa ajili ya kupitia yaliyojiri mwaka uliopita, kufanya maandalizi na kuwekana sawa kwa mwaka wa masomo 2013/14, ambao kwa vyuo vingi utaanza mwezi Oktoba, 2013.

Awali akifungua kikao hicho Mkurugenzi wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sylvia Temu, aliipongeza Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kwa utendaji wake mzuri wa kazi licha ya changamoto nyingi wanazokumbana nazo.

`Serikali inapongeza utendaji wenu mzuri wa kazi kwa mwaka wa masomo ulioisha kwani tumeshuhudia utulivu kwenye vyuo vyote na kwamba hakuna migomo iliyojitokeza. Aidha tunatambua changamoto ni nyingi lakini bado hamkukata tamaa katika kuleta ufanisi na kufikia malengo’’, alisema Prof. Temu.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. George Nyatega ameishukuru serikali kwa namna ambavyo imeendelea kuipa Bodi ushirikiano kwa kutoa fedha kwa wakati na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha utoaji wa mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wa elimu ya juu unafanyika kwa ufanisi..

Maafisa Mikopo walielezea changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika utendaji kazi wao ikiwemo ya ugumu wa kuwasilisha taarifa kwa mfumo unaopendekezwa na Bodi.

Katika kutatua tatizo hilo, Menejimenti ya Bodi imeandaa mfumo wa kompyuta utakaowezesha shughuli zote za uwasilishaji au upatikanaji wa taarifa za wanafunzi kupitia katika mtandao huo kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa pande zote zinazohusika na mikopo ya wanafunzi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages