Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akimkabidhi Bi. Magret Kaengea (kulia) shilingi milioni moja aliyojishindia katika droo ya promosheni ya Airtel Yatosha wiki hii. |
----------------------------------------------
Airtel kupitia promosheni yake kabambe ya Airtel Yatosha shinda nyumba 3 tayari imeshakabidhi jumla ya shilingi milioni 37/- taslim kwa wateja wake nchini.
Airtel leo ikiwa katika muendelezo huo wa kutoa zawadi imewazawadia washindi saba wa wiki hii kiasi cha shilingi milioni saba ambapo wateja 7 kila mmoja aliondoka na kitita chake cha shilingi milioni moja kufuatia droo iliyochezeshwa makao makuu ya airtel siku ya Jumatatu ya wiki hii.
Mmoja wa washindi walioibuka na kitita cha shilingi milioni moja ni Bw. Rashidi Hamis ambaye ni fundi wa magari aliyeeleza wazi kuwa hakutegemea kabisa kupata kiasi hicho cha fedha katika msimu huu na anamshukuru Mungu kwa Airtel kumchagua kama mmoja wa washindi hao.
“Nawashukuru sana Airtel, kwa pesa hii nitaitumia kwa ajili ya shughuli zangu binafsi za kimaendeleo na nategemea itaniendeleza kiuchumi kwa kuweza kuimarisha maisha yangu,” alisema.
Washindi wengine wa milioni moja ni pamoja na John Joseph kutoka Karatu, Gideon Rwegosora kutoka Tanga, Omari Abeid kutoka Shinyanga, Hamis Esia kutoka Dar es salaam, Godbless Kweka kutoka Mtwara na Magreth Kalengea kutoka Dar es salaam.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Airtel Bw. Jackson Mmbando alisema leo tunayofuraha kupata washindi wa promosheni ya Airtel yatosha na kuwakabithi zawadi zao. Washindi hawa wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kujishindia kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kwa kutumia huduma za Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi vyetu mbalimbali.
Wateja wa Airtel wanaweza kujishindia milioni moja kila siku kwa kupiga *149*99#, chagua 2, chagua kifurushi chochote cha siku, wiki au mwezi kitakacho kufaa. Kumbuka vifurushi hivi pia vitakuingiza moja
kwa moja kwenye droo ya Airtel Yatosha Mpaka sasa Airtel imetoa shilingi milioni 37 kwa washindi 37 na inaendelea na promosheni hiyo ambayo inadumu kwa siku 90.
Sambamba na hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni jijini Dar es Salaam bado zinashindaniwa kupitia promosheni ya Airtel yatosha baada ya moja kuchukuliwa na mshindi wa kwanza Bw. Silvanus Juma mkazi wa Iringa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)