Nyumba ya Baba Askofu Festo Daudi Ngowo
Nyumba ya Baba Askofu Ngowo ikionekana katika Pande zote 2
Nyumba ya Baba Askofu Ngowo ikionekana katika Pande zote 3
---
Na Bryceson Mathias, Dodoma
WAUMINI
wengi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya
Dodoma, wameguswa na kujitokeza kwa wingi kumchangia Ujenzi wa Nyumba ya
Askofu Mstaafu Festo Daudi Ngowo ambaye amefumbwa kinywa na hasemi.
Katika
Harambee rasmi iliyofanyika Jumapili iliyopita Julai 28, mwaka huu,
Sharika nyingi za Mjini Dodoma zilivuka Malengo malengo yao
waliyopangiwa na Uongozi wa Dayosisi, Majimbo, Sharika na Mitaa, ambapo
Usharika wa Iringa Road uliongoza kwa kutoa Mil. 2/-
Akizungumza
na Gazeti la Upendo Askofu Msaidizi Samweli Mshana aliwapongeza Waumini
wote wa Dayosisi kwa Ushirikiano Mkubwa wa Njia hii ya Kikristo, ambapo
alisema Utandazaji wa Mbao za Dari (Blundering) umekwisha na leo (Jana)
uwekaji wa Madirisha (Grill) unaanza mara Moja.
“Waumini
na Watumishi wote kwa ujumla wao wanataka kuteka Baraka, na ni kweli
tunakwenda kuziteka, kwa sababu waumini kila kona wamejguswa kujitolea
kumsaidia Askofu wao (Ngowo) kwa hali na Mali, Jambo ambalo
limetufurahisha sana Viongozi wa Dayosisi”.
Katika
Harambee hiyo, Mafundi wa Utandazaji wa Umeme wa Kanisa Kuu (Cathedral)
Dodoma na Ipagala KKKT walitolea bure kufanya kazi hiyo, huku Mwalimu
wa Veta na Mzee wa Kanisa la Ipagala Mtalaam wa Ufundi Bomba, pia
alijitolea kufanya kazi hiyo bure, na wengi walijitolea Malumalu
(Tiles).
Aidha
Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Amoni Kinyunyu, amewashukuru
waumini wote kwa kujitoa, na amewaomba wachungaji, Wainjilisti na
Ma-Parish workers wote, kuwakilisha fedha na Michango yote imfikie Kaimu
Askofu Mkuu Mshana na Kamati ya Ujenzi wa nyumba hiyo, tayari kwa
utendaji.
Hata
hivyo Kamati ya Ujenzi, inakusudia hadi mwezi wa Septemba Mwaka huu
Askofu Ngowo awe ameingia kwenye Nyumba hiyo, ili apumzike nyumanai pake
kwa kazi nzuri ambayo amemfanyia Mungu aliyemuinulia watu wa kumsaidia.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)