Afisa
Mipango wa MitOst Mete Odabasi akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Vijana kwa niaba ya Wizara ya Habari. Vijana, Utamaduni
na Michezo kufuatia ushirikiano waliopewa katika ziara yao hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na vijana
wanaojitolea kutoka Ujerumani ambao wapo nchini kufuatia mpango wao wa
kubadilishana rasilimali watu kupitia asasi ya kirai ya Tanzania Youth
Coalition leo jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizarani hapo.
Mmoja
wa wanachama wa Tanzania Youth Coalition (TYC) ambaye pia ni mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bibi Neema Kassala (kushoto) akichangia
mada walipokutana na Mkurugenzi wa Maendeleo yaVijana walipotembelea
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam
kufuatia kuwa wenyeji wa wageni kutoka Taasisi ya MitoSt ya jijini
Hamburg Ujerumani waliopo nchini.
Mmoja
wa wakilishi kutoka Taasisi ya MitOst yenye makao yake jijini Hamburg
Ujerumani Bibi Lusinja Czesnik (wa pili kutoka kushoto) akichangia mada
jana walipokutana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana leo jijini Dar es
Salaam walipotembelea Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo ili
kujifunza namna Serilikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya
vijana hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg
Ujerumani walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
kujifunza namna Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya Vijana
kupitia wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana na wawakilishi kutoka
taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani walipotembelea Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujifunza nama Serikali ya Tanzania
inavyoshughulikia masuala ya Vijana kupitia wizara hiyo jana jijini Dar
es Salaam. Picha Zote na Frank Shija wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)