UTURUKI YAKABIDHI GARI LA MAALUM LA KUCHUNGUZA MATUKIO YA UHALIFU KWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UTURUKI YAKABIDHI GARI LA MAALUM LA KUCHUNGUZA MATUKIO YA UHALIFU KWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali, Said Mwema (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya (katikati) wakisaini hati ya ushirikiano wa kuchunguza matukio ya uhalifu kati ya Tanzania na Uturuki. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akilishuhudia tukio hilolililofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiwashukuru kwa furaha ujumbe kutoka nchini Uturuki baada ya kukabidhi gari maalumu ya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini kwa Jeshi la Polisi. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini lilikabidhiwa leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiliwasha gari maalumu la kuchunguza matukio ya uhalifu mara baada ya kukabidhiwa ufunguo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini lilikabidhiwa leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (watatu kutoka kulia-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka nchini Uturuki pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kusaini hati ya ushirikiano wa uchunguzi wa matukio ya uhalifu kati ya nchi ya Tanzania na Uturuki. Jeshi la Polisi Uturuki tayari limekabidhi ya gari maalumu la kuchunguza hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages