Mkufunzi
wa kimataifa wa maswa ya mazoezi ya viungo bwana SAAS akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya tamasha kubwa
linalowakutanisha wafanya mazoezi kote nchini na familia zao
linalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar Es Salaa
ambapo watu mbalimbali watapata fursa ya kujumuika pamoja na kufanya
mazoezi ya pamoja sambamba na hilo pia burudani toka kwa bendi ya Twanga
pepeta na Roma Mkatoliki na baa za kisuma na Fyatanga zitakuwepo
kuchoma nyama kwa kipindi chote,Katikakati ni Meneja wa Vitamalt Plus
Consolata Adam na Meneja mawasiliano na mahusiano wa Tbl Edith Mushi
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
………………………………………………………………….
KATIKA kuhakikisha Watanzania
wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt,
kimeandaa bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi na
litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya, Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,
Meneja wa Vinywaji visivyo na Vileo katika Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), Consolata Adam alisema, wameamua kuandaa bonanza hilo ili
kuwakutanisha pamoja wafanya mazoezi wote, ambao mara nyingi wanafanyia
katika vituo maalumu (gym).
Consolata alisema, bonanza hilo la aina yake kwa Dar es Salaam litafanyika katika Viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama kuanzia saa 12 asubuhi hapo kesho (Jumamosi).
“Tumeamua kuandaa bonanza
linalowakutanisha wanamichezo mbalimbali hasa wafanya mazoezi ili kuweza
kukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja.
“Siku hiyo katika Viwanja vya Posta kutakuwa na gym kumi na mbili zilizo maarufu ambazo zitashiriki na kutakuwa na wakufunzi kumi ambao wataongozwa na mkufunzi wa kimataifa SAAS,” alisema, huku akidai mtu anatakiwa kwenda tu kwani mazoezi hayo yatakuwa bure.
Alisema, lengo kuu kuu la bonanza
ni kuhamasisha jamii nzima kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi ili
kujenga afya bora za miili yao na pia kujenga umoja imara wa gym
zilizopo nchini.
Consolata alisema, katika
kuhakikisha bonanza hilo linakuwa bora na la kufana jumla ya gym kumi na
mbili zitashiriki ambazo ni Better Life, Genessis ya Kijitonyama,
Segerea Gym, Rio Gym,Genessis ya Kimara, Azula ya Mikocheni na Serena
Gym.
Alisema pia baa zilizoshinda
katika kuchoma nyama katika mashindano yaliyofanyika hivi karibuni za
Fyatanga ya Tegeta na Kisuma Bar ya Temeke, zitaonyeshana umwamba kwa
kuchoma nyama bomba kwa kipindi chote hicho
“Tumeweka burudani za kila aina
kwani kutakuwa na michezo mbalimbali ya kufurahisha kama soka, netiboli,
kuvuta kamba, kukimbiza kuku, Sehemu za watoto kuchezea pia na zawadi
nyingi toka Vita Malt zitakuwepo.
NaYe Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TBL, Edith Mushi alisema
mbali na hayo kutakuwa na burudani mbalimbali toka kwa bendi African
Stars ‘Twanga Pepeta’ na msanii mkali wa Hip hop, Roma Mkatoliki
sambamba na burudani nyingine nyingi kwa kipindi chote cha tamasha.
“Hii ni siku ya familia napenda kuwajulisha watanzania wote na
wapenda michezo kote nchini kuwa waje mapema na familia zao siku ya
Jumamosi, hakutakuwa na kiingilio chochote na vinywaji vyote toka TBL
vitakuwepo.
“Lakini pia watu wa kawaida na wa rika zote siku hiyo hakutakuwa
na kikwazo chochote cha kufanya mazoezi, kwani ni bure kabisa, hivyo
nawashauri tufike kwa pamoja ili tuweze kupata pia ushauri mbalimbali
juu ya kupunguza uzito na aina ya mazoezi yanayotakiwa,” alisema
Vita Malt ni kinyaji kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)