Baadhi ya wapangaji wakitoa vyombo vyao chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi
Baadhi ya wapangaji wakiendelea kutoa vyombo vyao chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Mallya (kulia) pamoja na Ofisa Mkuu wa Programu na Utawala wa Fedha wa TGNP, Anna Kikwa (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari.
Mmoja wa maofisa wasaidizi kutoka kampuni ya udalali ya Mamba (katikati anayezungumza kwenye vinasa sauti) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kutoka vyombo anuai kuhusiana na kazi yao ya kuwaondoa kwa nguvu wapangaji hao.
Wapangaji wakitoa mizigo yao
Na The Habari.Com
MTANDAO
wa Jinsia Nchini Tanzania (TGNP) leo umefanikiwa kuwaondoa kwa nguvu
wapangaji ving'ang'anizi ambao walishindwa kesi ya kuligombea jengo la
ghorofa moja lililopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo ambalo TGNP ililinunua toka kwa mfilisi wa iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited (TSTML) yaani Benki ya Rasilimali ya Tanzania (TIB) mwaka 1997 lilikuwa likigombewa na wapangaji 21 ambao walifungua kesi Mahakama Kuu kupinga mchakato wa uuzwaji wa jengo hilo kwa TGNP.
Jengo hilo ambalo TGNP ililinunua toka kwa mfilisi wa iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited (TSTML) yaani Benki ya Rasilimali ya Tanzania (TIB) mwaka 1997 lilikuwa likigombewa na wapangaji 21 ambao walifungua kesi Mahakama Kuu kupinga mchakato wa uuzwaji wa jengo hilo kwa TGNP.
Zoezi
la kuwaondoa wapangaji hao limefanywa na dalali wa Mahakama, Mamba
(Mamba Auction Mart) kwa niaba ya TGNP chini ya ulinzi mkali wa polisi,
ambapo wapangaji waliogoma kuondoka wenyewe baada ya kushindwa kesi
walitolewa vyombo vyao nje ya jengo hilo na kuamriwa waondoke.
Mwandishi
wa habari hizi alishuhudia wafanyakazi wa kampuni ya udalali ya Mamba
wakitoa vyombo vya wapangaji nje ya jengo huku gari za polisi mbili
zikiwa na baadhi ya askari wenye silaha na mabomu ya machozi zikiwa nje
ya jengo hilo kuhakikisha hakuna anayegomea amri ya mahakama.
Kuondolewa
kwa nguvu kwa wapangaji hao kumekuja mara baada ya Jaji wa Mahakama
Kuu, Jaji Mwaikugile Machi 13, 2013 kutupilia mbali maombi ya wapangaji
hao na kuwataka waondoke mara moja.
"...Leo
hii zoezi linalotekelewa ni kutimiza amri ya Mahakama Kuu ya Machi 13,
2013 na amri ya mahakama ya kumpa ruhusa dalali wa mahakama Mamba
Auction Mart, na zoezi linafanyika chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi
kama mahakama ilivyoamuru," inaeleza taarifa ya TGNP.
Akizungumzia
tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Mallya alisema
wanashukuru kuona haki imetendeka na taasisi yao kuachiwa jengo hilo
ambalo walilinunua kihalali kutoka kwa mmiliki.
Alisema
TGNP italitumia jengo hilo kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kutanua wigo
wa taasisi zake za mafunzo ya kijinsia kwa jamii ikilenga kuwajengea
uwezo wa kutumia fursa zao kudai na kulinda rasilimali ili kujiletea
maendeleo.
Aliongeza
kuwa wapangaji hao wamekuwa wakilitumia jengo hilo takribani kwa miaka
16 bila kulipia gharama za huduma kama za maji na nyinginezo, huku
baadhi ya wapangaji kuwapangisha wapangaji wengine kinyemela na
kujipatia fedha
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)