Teknoljia ya mstari wa goli ajili ya Ligi Kuu ya Uingereza imezinduliwa
leo na kusifiwa kama moja ya maendeleo muhimu toka sharia za soka ziwekwe na kuanza kutumika miaka 150 iliyopita.
leo na kusifiwa kama moja ya maendeleo muhimu toka sharia za soka ziwekwe na kuanza kutumika miaka 150 iliyopita.
Teknolojia hiyo ijulikanayo kama ‘The Hawk-eye’ (jicho la mwewe) inatumia kamera 14 ambazo zitatuma ujumbe ndani ya sekunde moja katika saa ya mwamuzi pamoja na kifaa cha sikioni cha mawasiliano mara tu mpira utapovuka mstari wa goli.
Watumiaji wa kwanza wa kifaa hicho watakuwa timu za Manchester United na Wigan Jumapili ijayo katika mchezo wao wa ngao ya hisani kuashiria kuanza rasmi kwa ligi hiyo katika uwanja wa Wembley.
Cheki Video hii ya jinsi kifaa hicho kitavyofanya kazi
Chanzo Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)