TAMASHA LA SERENGETI FIESTA KUTUA MTWARA MARA YA KWANZA JUMAMOSI HII - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA KUTUA MTWARA MARA YA KWANZA JUMAMOSI HII

Wasanii maarufu wa kizazi kipya zaidi ya Kumi tano watatoa burudani kwa mara ya kwanza kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara na majirani zake katika tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2013 ambalo ni maarufu kwa ”Tupo Pamoja, Twenzetu, Tukawinde” Ni Noma sanaa” litalofanyika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo mjini Mtwara. Burudani hiyo itakuwa kivutio tosha kwa wakazi wengi kutokana na kundi kubwa la wanamuziki wa kizazi kipya waliopo kwenye chati za juu katika muziki huo.
 Tamasha hilo linaambatana na shamrashamra zinazoendelea kwenye promosheni za bar mjini hapo ambapo wakazi wa Mtwara watakuwa wakijishindia tiketi za bure pamoja na fulana baada ya kujibu maswali marahisi, pia kutakuwa na washindi ambao watapata nafasi ya kuwakilisha Mtwara kwenye tamasha la kuhitimisha msimu wa Fiesta 2013 jijini Dar Es Salaam. 
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager ambayo ndio bia inayodhamini tamasha hili kubwa, Allan Chonjo alisema ”Mpaka sasa tumepata wawakilishi kumi na moja Lydia Bitwale, Belinda Mgongorwa, Samweli Aloyce, Josiah Naftael na Severine Matata kutoka Kigoma, Issa Jaffary, Jayson Baduga na Augistino Massawe Kutoka Tabora na Singida ni Richard Mmassy, Emmanuel Nagunwa na Rose Tarimo”.

 ”Washindi wote kutika mikoani watakaa jukwaa la watu maalumu ambapo wataweza kushuhudia burudani kwa karibu zaidi na watapata nafasi ya kupiga picha na wasanii wakubwa, hivyo tunawaomba wakazi wa
Mtwara waendelee kunywa bia ya Serengeti  ili waweze kujishindia bia za bure na hatimaye kushinda nafasi hiyo ya kuja Dar Es Salaam kwa ajili ya Fiesta ya mwisho”. Wateja wanatakiwa kuangalia chini ya kizibo na kuona kama wajishindia bia za bure kwani kuna bia zaidi ya laki mbilli nchi nzima,  aliongeza Chonjo.

Msanii mkali katika miondoko ya kipwani Snura, ambaye ni maarufu kwa wimbo wake wa ”majangaa” ataungana na wasanii wengine waliofanya vizuri kwenye tamasha hilo lililoanzia mkoani Kigoma ambapo ilikuwa kwa mara ya kwanza pia, ikafuatiwa na Tabora na Singida wikiendi iliyopita. Wasanii zaidi ya kumi na tano wanaokubalika kama Nay wa Mitego, Makomandoo, Juma Nature, Matonya, Kassim Mganga,  Chege na Temba, Snura, Madee, Young Killer, Stamina, Godzilla, Nikki Wa Pili, Ommy Dimpoz, Kalapina na Pasha ambaye anatokea mkoani Mtwara watapanda jukwaani kukonga nyoyo za wakazi wa mji wa Mtwara siku ya Jumamosi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages