SHULE YA MZUMBE SEKONDARI WANUFAIKA NA MRADI WA TEHAMA KUTOKA KOICA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SHULE YA MZUMBE SEKONDARI WANUFAIKA NA MRADI WA TEHAMA KUTOKA KOICA

 Meneja Mradi wa Shirika la Kimataifa La Maendeleo La Korea (KOICA)  Bw Kim Seong Su wa pili kutoka kushoto Akiimba Wimbo wa Taifa Pamoja Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Joseph Kuzirwa Wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Tehama Katika Shule ya Sekondari Mzumbe Wilaya ya Mvomero Morogoro.
  Meneja Mradi wa Shirika la Kimataifa La Maendeleo La Korea (KOICA)  Bw Kim Seong Su Akizungumza katika Uzinduzi huo ambapo alisisitiza Mradi huo uwasaidie wanafunzi katika kupata maarifa zaidi kwenye masomo yao ili shule hiyo iweze kuendelea kuwa moja ya shule bora kitaaluma hapa Nchini .
Mgeni Rasmi Makamu  Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Joseph Kuzirwa akishukuru Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Korea (KOICA) Kwa Msaada huo,Prof. Kuzirwa alisema kuwa huo ni mradi wa majaribio lakini baadaye utapelekwa katika shule zingine hapa nchini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanafunzi wa Sekondari hasa zile zilizokuwa mbali na miji ambazo zinakosa fursa ya kutumia mfumo wa ICT hivyo baada ya kufika kwa mradi huo shuleni hapo wanafunzi kupata maarifa ya kitaaluma.
Meneja Mradi wa Shirika la Kimataifa La Maendeleo La Korea (KOICA)  Bw Kim Seong Su wa pili kutoka kulia Pamoja Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Joseph Kuzirwa anayefuatia wakizindua Mradi shuleni hapo.Picha Na .MATUKIO NA MICHAPO BLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages