SABABU ZA MICHAEL WAMBURA KUUNGA MKONO UAMUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO NA VILABU KUKATAA KUSAJILI MAREKEBISHO YA KATIBA YA TFF KUTOKANA UKIUKWAJI WA UTARATIBU NA SHERIA ZA MAREKEBISHO YA KATIBA TFF 2013 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SABABU ZA MICHAEL WAMBURA KUUNGA MKONO UAMUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO NA VILABU KUKATAA KUSAJILI MAREKEBISHO YA KATIBA YA TFF KUTOKANA UKIUKWAJI WA UTARATIBU NA SHERIA ZA MAREKEBISHO YA KATIBA TFF 2013


Katiba ya TFF ya 2012 ilifutwa na msajIli wa vyama vya michezo na vilabu kwa kuwa ilibadilishwa kinyume cha sheria(BMT)  pamoja na Katiba ya TFF ibara ya 30  kwa kutumia njia ya waraka badala ya Mkutano Mkuu,  hivyo katiba halali kisheria inayotambulika ni ile ya 2006 na mabadiliko yake . FIFA  na Serekali kupitia wizara yenye dhamana na  michezo iliiagiza  TFF iitishe Mkutano Mkuu ili ifanye mabadiliko ya katiba stahiki kwa mujibu wa katiba  na  kwa kufuata taratibu zilivyoainishwa  kwenye katiba ya TFF. Nimelazimika kuendelea kuiunga mkono Serikali kupitia  msajili  kwa maamuzi yake ya kukataa kusajili mabadiliko  ya katiba ya TFF kwa kuwa TFF  kwa makusudi   imeendelea kuvunja katiba yake katika kufanya mabadiliko.
Kisheria  msajili husajili mabadiliko yoyote ya Chama kilichosajiliwa chini ya Sheria ya BMT kwa kuzingatia  Sheria NA 12 ya 1967 na marekebisho yake NA 6 ya 1971 ya Baraza la Taifa la Michezo pamoja na  Kanuni za Baraza la Michezo la Taifa  na Kanuni za  Usajili NA 422 za1999.
 Chama chochote kitakacho kwenda kinyume na sheria hizo hikiwezi kupewa usajili au Katiba yake na marekebisho yake hayawezi kupewa usajili,aidha uamuzi wa msajili   sio tu utaifanya TFF peke yake itambue sheria  bali hata vyama vingine vitawajibika kufuata utaratibu katika kufanya mabadiliko ya katiba zao,
Katiba ni nyaraka ya kisheria hivyo chombo chenye mamlaka kisheria hapa Tanzania ya kutafsiri katiba ni Mahakama pale pande mbili zinapotofautiana juu ya tafssiri ya Katiba, hivyo kwa kufanya hivyo msajili atakuwa ameepusha suala la Katiba ya TFF kuingia katika mikono ya kimahakama kwa kuwa utaratibu uliotumika kubadili katiba ya TFF  ni dhahiri haukufuata taratibu zilizoainishwa kwenye katiba ya TFF  na sheria na  za nchi kama zilivyoaanishwa. Sababu kuu zinazonipelekea mimi kuunga mkono uamuzi huo ni kama zifuatazo:

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages