Meneja
Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rugambo Rodney akimkabidhi funguo mbili
Diana Elis Mkoba baada ya kushinda shindano la Tamasha la Serengeti
Fiesta 2012. Diana alikabidhiwa magari mawili aina ya Vitz yenye thamani
ya shs milioni 18.Katikati ni Baba mdogo wa mshindi, Gratian Mkoba
ambaye ni Rais wa chama cha Walimu Tanzania (CWT). Mwaka huu, Kampuni
hiyo itatoa magari manne, pikipiki 12 na fedha taslim shs 100,000 ikiwa
juma ya zawadi zote ni sh million 80.
********************************************
KAMPUNI
ya Push Mobile Media Limited itatoa zawadi za magari aina ya Vitz manne
(4) na pikipiki 12 kwa mashabiki mbali mbali watakaoshinda bahati
nasibu maalum ya tamasha la Serengeti Fiesta linalotarajiwa kuzinduliwa
Jumamosi mjini Kigoma.
Meneja
Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa
zawadi mbali ya magari na pikipiki, pia watatoa zawadi za fedha taslim
(sh 100,000) kwa mashabiki hao ambao ili kushinda wanatakiwa kutuma neno
Fiesta kwenda namba 15678 ili kuweza kushinda gari, pikipiki au fedha
taslim na unaweza kushinda tiketi ya VIP kwa kutuma jina la msanii kwa
mfano Diamond na kuacha nafasi na baadaye kuwema maoni yako kwenda namba
hiyo hiyo.
Rodney
alisema kuwa mbali ya kushinda tiketi, mshiriki atalipiwa tiketi ya
ndege kuja Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la fiesta
la mwisho. Alisema kuwa wameamua kuweza zawadi hizo nono ili kunogesha
zaidi tamasha hilo ambalo kwa kuwanufaisha mashabiki wa muziki hapa
nchini.
Aliongeza
kuwa wamejipanga ili kuwashirikisha wananchi wote katika tamasha hilo
kwani watatoa pia watazindua huduma mpya ijulikanayo kwa jina la Simu TV
ambapo itamwezesha mashabiki kuona video mbali mbali za muziki na
matukio mengine, kupata nyimbo mbali mbali, kupata taarifa mbali mbali
ikiwa pamoja na za michezo kwa kupitia simu ya mkononi.
kuhusiana
na zawadi za fedha, Rodney alisema kuwa zawadi hiyo itakuwa inatolewa
kila siku kwa mashabiki watakaoshinda bahati nasibu hiyo. Alifafanua
kuwa jumla ya sh milioni 80 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi
hili litakalodumu kwa kipindi cha miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)