baadhi ya wanafunzi wakiwa mbali na shule hiyo wanacheza
mwalimu Agostino akizungumzia jambo linalowafanya watoto kutojua kusoma wala kuandika shuleni hapo
mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makumbusho akizungumza na wazazi katika kikao cha kujadili maendeleo ya wanafunzi shuleni hapo
wazazi walioitikia wito wa kikao hicho.
Mwa limu mkuu wa shule ya msingi makumbusho mama lyimo leo aliitisha kikao cha kujadili maendeleo ya wanafunzi shuleni hapo na hasa wale wasiojua kusoma na
kuandika. Hii ni katika mikakati aliyojiwekea kwa kufanya mikutano ya wazazi na
walimu wa madarasa mara kwa mara kujadili maendeleo ya mwanafunzi shuleni hapo.
Mama lyimo alilaani
vikali vitendo vya baadhi ya wanafunzi kutojua kabisa kusoma na pindi wazazi
wanapoitwa kutotoa ushirikiano, kuhusiana na hilo ameahidi mwakani kutopokea mwanafunzi wa darasa la kwanza asiyepitia
shule za awali(chekechea) na atawatimua
wale wanafunzi wasiokuwa na maendeleo mazuri na wazazi hawataonesha
ushirikiano.
Wakati huohuo katika kikao hicho baadhi ya
wazazi walilalamikia walimu kutokuwa makini madarasani na kuwalazimisha watoto wabaki
tuisheni, na kupelekea wale watoto wasiosoma tuisheni kukosa masomo
kamilifu kwani masomo yote hufundishwa zaidi tuisheni na sio madarasani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)