Baadhi ya
wachezaji wa Klabu ya Mpo Afrika wakishangilia na Kikombe mara baada ya kuibuka
mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa,Mkoa
wa Temeke iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mpo Afrika ilishinda
13-11 dhidi ya Klabu ya Sun City.
Katibu Mkuu
wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga akimkabidhi zawadi ya fedha
taslimu shilingi 350,000/= bingwa wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles),
Sulemani Cato mara baada ya kumfunga Nahodha wa timu ya Taifa Charles Venance
4-2.Dar es Salam mwishoni mwa wiki.
Mchezaji wa
timu ya Klabu ya Mpo Afrika na Nahodha wa timu ya Taifa, Charles Venance
akicheza wakati wa mechi ya fainali dhidi ya klabu ya Sun City wakati wa
mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Temeke iliyofanyika
mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi
Wetu.
TIMU ya Mpo Afrika ya Mkoa wa
kimichezo ya Temeke jijini Dar es Salaam imetwaa ubingwa wa mkoa baada ya kuifunga
timu ya Klabu ya Sun City 13-11, katika fainali za mashindano ya mchezo
wa Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa Klabu ya Bushnet Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam.
Mpo afrika kwa ushindi huo
ilizawadiwa Kikombe, fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya
kuwakilisha Mkoa wa Temeke katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika
mwezi ujao Mkoani Morogoro.
Nafasi ya pili ilichukuliwa
na klabu ya Sun City na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000/= na
nafasi ya tatu katika mashindano hayo ilichukuliwa na Klabu ya Kurasini ambayo
ilizawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000/= na mshindi wa nne ni klabu ya Bushnet ambao
ndio walikuwa wenyeji wa mashi ndano hayo.
Upande wa mchezaji mmoja
mmoja wanaume(Singles), Mchezaji waKlabu ya Bushnet, Sulemani Kato(Shetani)
alifanikiwa kuchukua ubingwa kwa kumfunga Charles Venance 4-2 na kujinyakulia
zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa
wa kimichezo wa Temeke katika fainali za kitaifa Mkoani Morogoro.
Nafasi ya pili ilichukuliwa
na mchezaji Charles Venance kutoka klabu ya Mpo Afrika ambapo alizawadiwa fedha
taslimu shilingi 200,000/= na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mchezaji,
Amos Boniphace ambaye alizawadiwa 150,000/= na nafasi ya nne ni Hassan
Abdubakar.
Upande wa mchezaji mmoja
mmoja wanawake (Singles), Beatrice Charles alitwaa ubingwa kwa kumfunga Madina
Idd 4-0 na hivyo kujinyakulia zawaadi ya fedha taslimu shilingi 250,000/=
pamoja na tiketi ya kwakilisha mkoa wa Temeke katika fainali za kitaifa mkoani
Morogoro.
Madina Idd ailichukua nafasi
ya pili na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/= .Nafasi ya tatu
ilichukuliwa na Manka Mushi ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 100,000/=
na nafasi ya nne ni Rebeka Magaigwa ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi
50,000/=.
Akizungumza na wachezaji
kutoka vilabu vyote, Katibu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga
aliwaomba klabu iliyotwaa ubingwa na ambayo itawakilisha mkoa wa Temeke katika
fainali za kitaifa mkoani Morogoro kujiandaa vyema kwani ushindani ni mkubwa huko
wanakoelekea na pia wazingatie nidhamu kwani bila nidhamu inaweza kuwafanya
wasifanye vizuri mbele ya safari.
Mwisho aliwshuikuru TBL,
kupitia bia ya Saafari Lager kwa kuendelea kufadhili mashindano hayo ambapo
aliwaomba wapenzi wa pool kunywa Safari Lager ili waendelee kuwa wafadhili
wakuu wa mashindano ya Pool.
Mashindano ya Safari Pool
Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni ulishirikisha vilabu tisa ambavyo ni Mpo Afrika,
Sun City, Kurasini,Bashnet,BMK,Sifa Mtoni,MTN,Amazoni na SuperStar.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)