Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA
wa Chelsea, Mreno Jose Mourinho amesema atapigana kufa na kupona mpaka
siku ya mwisho katika jaribio lake la kumsajili mshambuliaji wa
Manchster United, Wayne Mark Rooney majira haya ya kiangazi.
Chelsea
yenye makazi yake darajani , jijini London, tayari walishatuma ofa
mbili ambazo zimekataliwa na Manchester United, ofa ya mwisho
inayotajwa kuwa ni zaidi ya paundi million 25 ilitumwa jumapili. Lakini
Mourinho alisema: “Hatuna kizuizi cha muda kwenye suala hili.
‘Tumemuona
Rooney ni mchezaji ambaye tungependa kuwa nae. Tumefanya kila kitu kwa
utaratibu unaopaswa na tutafanya hivyo mpaka siku ya mwisho ya usajili”.
Alisema Mourinho.
Rooney
inaaminika kwamba amemwambia kocha wake David Moyes kwamba anataka
kuondoka, lakini United imekuwa ikisisitiza kwamba hauzwi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)